Breaking News

MBETO ATABIRI ACT KUSAMBARATIKA ZANZIBAR

Mwandishi Wetu , Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetabiri licha ya ACT Wazalendo kuwa kitashindwa Uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka huu, kuna dalili zote za kufa mikononi mwa uongozi wa Mwenyekiti Othman Masoud Othman na Makamu wake, Ismail Jussa Ladhu .

Hakiwezi kufika popote baada ya idadi kubwa ya wanachama wa ACT kuchoshwa na uongozi wa kidikteta na kebehi za Jussa.

Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamisi, aliyedai kuna dalili ya ACT kufikwa kwa mwisho mbaya wa uongozi chini ya viongozi hao wawili.

Mbeto alisema ikiwa baadhi ya wanachama waasis na vigogo wa ACT katika ngazi mbalimbali wanakilalamikia chama chao kuendeshwa kidikteta ,dharau na kiburi, chama hicho kinaweza kukatika na kufa.

Alisema kuna wanachama ambao wameanza kuhoji kwanini Othman apewe uongozi wa juu wakati alikataa kukiunga mkono CUF na kutoshriki harakati za upinzani na wakati wote alikuwa mtumishi mtiifu SMZ.

"Jussa na Othman kaeni kwa makini chama kitawafia mikononi mwenu. Historia ya ACT itawaandika kwa wino wa machozi ya aibu. Hamtakiwi ndani ya ACT anzeni kujitafakari upya "Alisema Mbeto. 

Aidha Katibu huyo Mwenezi, alisema kikundi cha watu saba ndani ya ACT ambao ndio wanaopitisha maamuzi yote kuliko katiba ya ACT, baadhi ya wanachama wanapinga aina ya uongozi usiozingatia maamuzi ya pamoja.

"Kuna wanachama wengi wanataka kurudi CUF . Madai yao hawamtaki Jussa .Wanahoji alikopata utajiri wakati hana kazi wala biashara .Othman ajipime kama unatosha ili asifikwe na fedheha kwa dhambi za Jussa " Alisisitiza 

Mbeto alidai tokea Mwaka 1992 ,Othman aliitwa na Hayati Maalim Seif Sharif Hamad ili akiunge mkono CUF akakataa hivyo hakuna sababu yoyote ya kupewa madaraka ya juu ACT. 

"Madai ya Jussa kusema Othman alipendekezwa toka wakati wa uhai wa hayati Maalim seif , ni hadithi ya kutunga na uongo. Haiwezekani Maalim Seif amtaje Othman na kuwaacha kina Juma Duni au Mohamed Dedes " Alieleza

Hata hivyo baadhi ya wanachama wa ACT wamekasirishwa na uamuzi wa kikundi cha watu saba ACT kuanza kumpigia debe la kugombea urais wa Zanzibar Othman kabla ya kufanyika maamuzi ya vikao vya kikatiba

No comments