MIMEA VAMIZI NI TISHIO KWA IKOLOJIA YA HIFADHI ZETU, BALOZI POLEPOLE
Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humprey Polepole amesema uwepo wa mimea vamizi katika maeneo yaliyohifadhiwa inaathiri na kubadilisha ikolojia ya maeneo hayo hali ambayo inapelekea kutoweka kwa nyanda za malisho ya Wanyamapori.
Mhe. Balozi Polepole aliyasema hayo leo tarehe 19 Februari, 2025 katika tambarare za Ndutu baada ya kuungana na timu ya watafiti kutoka Cuba na Tanzania wanaondelea na ziara yao ya kitafiti kuhusu mimea vamizi ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Aidha Mhe. Balozi Polepole alieleza kuwa maelekezo ya Serikali ni kutafuta suluhu ya kudumu ya mimea vamizi huku ikilenga kubadilisha mimea hiyo kupata bidhaa ambazo ni rafiki kwa matumizi ya binadamu ikiwemo mimea dawa (Medicinal plants).
Hata hivyo mimea vamizi ambayo imeonekana na watafiti hao ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ni pamoja na Parthenium hysterophus (Gugu karoti, Gutenibergia cordifolia (Gutenbergia).
Watafiti hao wamehitimishwa ziara yao katika Hifadhi ya Ngorongoro ambapo timu ya watafiti hao walitembelea baadhi ya maeneo ya Kayapus, Kakesio na Tambare za Ndutu.
No comments