Breaking News

NLD KUTOKUSHIRIKIANA NA VYAMA VINGINE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Dar es salaam - Chama Cha National League for Democracy (NLD) kimesisitiza kuwa hakina mpango wa kushirikiana na chama kingine chochote cha siasa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu 2025.

Akizungumza mapema leo februari 23, 2025 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati kuu jijini Dar es salaam katibu mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo amesema kwa mujibu wa yaliyotokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 mara baada ya kushiriki na kuungana na vyama vingine kupitia umoja wa UKAWA chama hakipo tayali kushirikiana na chama chochote kwa sasa.

"Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 chama chetu kilikuwa moja ya vyama vilivyoshiriki kuunda umoja wa UKAWA na kuzunguka kufanya kampeni nchi nzima kwa kutoa mda, asilimali zetu lakini baada ya kutangazwa kwa matokeo chama akikuweza kupata faida yoyote zaidi ya kuwanifaisha wengine kwa kupata wabunge na madiwani nchi nzima". Alisema Doyo

Alisema kufatia madhira hayo na siku za hivi karibuni kumekuwepo na tamko la CHADEMA lililotolewa kupitia Mwenyekiti wake Tundu Lissu "No reforms, no election" NLD haitaunga mkono msimamo huo, nabadala yake itajikita katika kuwatangazia wananchi sera zake ili kupata lidhaa ya kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Doyo aliongeza kuwa Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini vipo 19, ikiwemo chetu cha NLD, sisi hatuendi kwa msituni wala hatususii uchaguzi, bali tunaenda kuwaeleza wananchi sera za chama chetu ili kupata lidhaa ya kuongoza.

"kelele Zote zinazopigwa kuhusu kushirikiano ni unafiki, chama kitakachokuja kutuambia tujiunge kuiondoa CCM, chama hicho tunakiona ni adui yetu namba moja kwani tulishawahi kushirikiana nao kupitia UKAWA lakini hatukuwahi kunufaika na Muungano huo wa kisiasa". Alisema Doyo na kuongeza kuwa

"Ili Muungano uwe wenye tija kwa vyama vyote ni lazima uweke wazi na pasi na shaka kuhusu namna kila chama kitakavyonufaika baada ya uchaguzi na mgawanyo wa haki wa majimbo kwa vyama vya siasa ili kila chama kinufaike".
Awali akizungumza wakati akifungua mkutano wa kamati kuu ya chama hicho, Mwenyekiti wa chama NLD Taifa, Mfaume Khamis Hassan amewaasa Watanzania kuendelea kudumisha amani ya nchi na kuviepuka vyama vya siasa ambavyo vimekua vikichochea uvunjifu wa amani Nchini.

"Nitoe rai kwa wananchi kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano tulionao nchini hasa kipindi hiki tukielekea katika uchaguzi mkuu kwa kuviepuka vyama vya siasa ambavyo vimekua vikionyesha wazi kuwa na ajenda za kuchochea uvunjifu wa amani Nchini". Alisema Hassan.

Katika hatua nyingine Bw. Hassan ametoa Serikali kuchukua hatua za makusudi kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kuwapatia ajira ya kudumu walimu wanaojitolea.

Alisema walimu hao wamekuwa wanafanya kazi kubwa hivyo nitoe rai kwa serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan iwangalie kwa jicho la kipekee na kutatua changamoto hiyo kwa kuwapatia ajira za kudumu.

No comments