SHIGONGO: WATANZANIA TUMUUNGE MKONO DKT. SAMIA
Dar es salaam - Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Erick Shigongo ametoa pongezi na kuwataka watanzania kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa na dhamira ya dhati katika kuwaletea maendeleo wananchi kwa kutekeleza miradi mbalimbali na kufanya maboresho makubwa hasa katika sekta ya elimu, afya na miundombinu.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam amesema katika kipindi Cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dokta Samia Jimbo lake limekuwa ni moja ya majimbo yenye maendeleo kwani Jimbo limepokea bilioni 63 ambapo zimetumika katika ujenzi .
"Mimi kama Mbunge wa Jimbo la Buchosa nimepokea bilioni 63 ambazo zimetolewakatika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Barabara, Vituo vya afya 5, Shule za sekondari zaidi ya 8, Zahanati 21 na madarasa ya kutosha hivyo kufanya maisha ya wakazi wa Buchosa kuwa na mafanikio makubwa
Amesema pamoja dunia kipitia kipindi cha kuyumba kwa uchumi kufatia janga la ugonjwa wa COVID 19 lakini Tanzania ni moja ya nchi ambayo imepambana kurejesha uchumi wake kufikia asilimia 5 na kuwa moja ya mataifa yenye uchumi mzuri hivyo watanzania wana kila sababu ya kujivunia uongozi wa serikali inayoongozwa rais Dkt. Samia kwa jitihada zake na hatua za makusudi ambazo amekuwa akizichukua kukuza uchumi wetu
Ameongeza kuwa Tanzania ni nchi tajiri sana kwa rasilimali ikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya Almasi, Tanzanite na Madini mengine huku katika sekta ya utalii ikiwa ni nchi ya pili duniani baada ya Brazil na nchi ya kwa Afrika nzima katika sekta ya utalii, hivyo watanzania wanapaswa kutembea vifua mbele.
"Nilizungumza kule New York,Marekani kuwa Afrika ni bara lenye utajiri mkubwa wa rasilimali lakini imeshindwa kubadilisha rasilimali hizo kuwa fedha lakini kwa uongozi bora wa nchi yetu Tanzania,Sasa tunatumia utajiri wetu kujiletea maendeleo na Rais Dkt Samia ameamua kutumia utajiri huo kuanza na sekta ya utalii ambao kwa Sasa unaingiza fedha nyingi na pia anaitumia sekta ya Kilimo katika kukuza kipato". Alisema Mhe Shigongo.
Amesema sisi kmaa watanzania tumuunge mkono Rais Dkt Samia kwa kuhakikisha wanashiriki vyema katika kuchangia Pato la Taifa (GDP) kupitia sekta mbalimbali za uchumi ili kuendelea kukuza uchumi Wetu na kuongeza kuwa kama Tanzania itaenda kama ilivyo hivi Sasa basi baada ya miaka 15 itakuwa ni miongoni mwa mataifa tajiri zaidi duniani.
Akizungumzia kuhusu mipaka ya kibiashara barabi Afrika, Mhe. Shigongo amesema ni wakati bara la afrika kuamka na kuwa wamoja huku akilitolea mfano Taifa la Marekani ambalo halina mipaka kwenye majimbo yake kibiashara hivyo ni wakati kwa waafrika kuwa kitu kimoja kwa kukataa kuchonganishwa na nchi za Afrika zifanye biashara zenyewe kwa zenyewe na kuepuka kutumia fedha nyingi kuagiza bidhaa kutoka nje badala ya kununua bidhaa za nchi nyingine ndani ya bara hilo.
"Huu ni wakati wa Waafrika kufanya biashara kwa ushirikiano lakini Afrika hatufanyi hivyo kwa hiyo ni wakati wetu Sasa kuamka na kukataa kuchonganishwa ila kuwa wamoja",. Alisema Mhe. Shigongo
No comments