Breaking News

Dr Mayunga: Vyama Vya Siasa Vishiriki katika Mambo Muhimu Yenye Tija Kwa Taifa na Kuachana na Sababu ambazo Siyo za Msingi

Taasisi ya Right Way imevishauri vyama vya siasa nchini kushiriki katika mambo muhimu na yenye tija kwa Taifa na kuachana na  sababu ambazo siyo za Msingi.

Akizungumza na Mtandao huu katika mahojiano maalumu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dr.Wallace Mayunga alisema kwamba vyama vya siasa vimekua vikijikita katika kuibua agenda zisizo za maslahi kwa taifa kwa lengo la kuwadaa wananchi.

Alisema kwa mujibu wa matukio ambayo yamekuwa yakitokea kuonyesha wazi kuwa vyama vingi vya siasa nchini vimekua vitanguliza ajenda zao binafsi hasa katika mambo muhimu ya kitaifa mfano hivi karibuni vyamba vya siasa vya upinzani kutohudhulia hafla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwasilisha ripoti ya uchaguzi mkuu wa 2020.

"Baadhi ya Vyama vimetoa sababu, vingine vinadai Nec siyo tume huru, vingine vikadai hakukua na uchaguzi wa uhuru na haki, vingine vikatoa sababu kadha wa kadha lakini ukija kwenye uhalisia vyama vingi vya siasa hasa vya upinzani vinashindwa kupata matokeo mazuri kutokana na uwezo wake wa kifedha kuwa mdogo, Demokrasia mbaya ndani ya chama, pamoja na maandalizi ya kimkakati kuviwezesha kushiriki na kuibuka na ushindi" alisema Dr.Mayunga.

Alisema imeibuka tabia kwa baadhi ya vyama vya siasa  inapotokea kushindwa katika uchaguzi wowote kuaanzisha agenda na sababu za kuwafanya wananchi waone vimeonewa, kitu ambapo siyo jambo la msingi naviomba vyama hivi kuhakikisha vinafanya mambo sahihi ili vipate imani kwa wananchi wake.

Dr. Mayunga aliongeza kuwa taasisi yake imekua ikitoa elimu kuhusu mambo mbalimbali kususani masuala ya siasa na demokrasia ili kuvifanya vyama hivo viweze kujua misingi mbalimbali ya siasa nakuvifanya viweze kufanya vizuri katika chaguzi mbalimbali.

 

No comments