Breaking News

Millinga: Bado Mwamko ni Hafifu Usomaji wa Vitabu Nchini

Watanzania wameombwa kupenda kujisomea vitabu ili kuwafanya waweze kua na maarifa mbalimbali yatakayowasaidia kukabiliana na mambo mbalimbali katika maisha yao.

Akizungumza katika maonyesho ya Vitabu yanayoendelea katika ukumbi wa Makumbusho ya taifa posta jijini Dar es salaam,
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya A+ Communications
Bw. Humphrey Millinga alisema lengo kubwa la maonyesho hayo ni kuifanya jamii ipende kusoma vitabu.

Alisema kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika nchini zinaonyesha kuwa jamii ina mwako hafifu wa kujisomea vitabu hivyo kampuni hiyo imeona ni vyema kuandaa maonyesho hayo ili kusaidia jamii kutembelea viwanja vya makumbusho nakujionea aina mbalimbali ya vitabu na kuwafahamu waandishi wa vitabu hivyo.

Hata hivyo Millinga ameiomba jamii kubadilika nakupenda kujisomea vitabu ili waweze kupata maarifa mbalimbali pamoja na birudani ya hadithi mbalimbali.

"Haya ni maonyesho ya kwanza ambapo tutaendelea kuandaa mengine, lengo letu ni kuifanya jamii iwe na utamaduni wakupenda kusoma vitabu,hivyo haya maonyesho yatasaidia sana kuifanya jamii ibadilike, tunaomba wananchi na watoto wao wajitokeze kwa wingi"alisema Millinga.

Bw Millinga aliongeza kuwa hafla ya kufunga maonyesho hayo ya siku tatu atakuwa mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya taifa,  Dkt Noel Lwoga ambapo pia yanatarajia kuendelea kufanyika kila mwaka.

Nae mshiriki wa maonyesho hayo kutoka Taasisi ya Kuhamasisha usomaji wa Vitabu Tanzania (READ Tanzania), Bi. Lusekelo  Mwalughelo alisema mwitikio wa jamii katika maonyesho ya mwaka huu kutembelea mabanda na kujionea vitabu ni mdogo.

"Kutokana na maonyesho haya kua ni mara yake ya kwanza jamii bado haina uwelewa lakini kadri maonyesho hayo yatakavyokua yakiendelea yatawafanya watanzania wengi wapende kujisomea vitabu, tunaiomba jamii ipende kusoma vitabu, iwe na utamaduni wa kusoma muda wote na sio siku za mitihani tu au usaili fulani"amesema Bi Lusekelo

Alisema Taasisi ya RED imekua ikijihusisha na mradi wa utengenezaji wa maktaba na ugawaji wa vitabu mashuleni (Library Refurbishment project) ambapo shule 133 tayali zimenufaika na mradi huu, pia bado taasisi yetu inaendelea kuzisaidia shule zingine, natumaini kupitia maonyesho haya tutaendelea kutambulika zaidi.

No comments