Breaking News

Serikali Yashauriwa kutoa Elimu Juu ya Sera Na Miongozo Ya Uzalishaji Kwa Jamii Kuhusu sekta ya Uwekezaji wa Kilimo

SERIKALI imeshauriwa kufanya mapitio ya sera miongozo ya uzalishaji, pamoja na kuongeza jitihada za kuelimisha jamii masuala ya sekta ya Uwekezaji wa Kilimo likiwa na lengo la  kusaidia kuepukana na janga la uhaba wa chakula katika Taifa letu.

Ushauri huo ameutoa jijini Dar es salaam katika Kikao cha Wadau wa chakula Mwenyekiti wa Wabunge Vinara wa usalama wa chakula -(FoodSafety) Mbunge wa viti maalumu  Neema Lugangira ambapo alisema serikali haina budi kuboresha mifumo ya chakula kuanzia kwa Wazalishaji, Watunzaji kwenye Maghala na Walaji kwani chakula lazima kiangaliwe ili Afya ziwe bora.

Sanjari na hayo amesema Nchi ya Tanzania bado kuna baadhi ya maeneo yanakabiliwa na uhaba wa chakula kitu kinachosababisha wengi watoto kuwa na udumavu na utapiamlo katika ukuaji wao kutokana na vyakula wanavyokula hivyo kupitia kikao hicho na Mkutano Mkuu wa Chakula unaotararajiwa kufanyika Septemba mwaka huu katika jiji la New York Nchini Marekani wawakilishi watakaokwenda watakuja na suluhisho .

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira Clara Makenya amesema kuwa kwa wakati wa sasa kilimo kimekuwa kikiyaathiri mazingira kutokana na Wakulima wengi matumizi ya madawa na Viatilifu kwa wakulima wengi hali inayopelekea  ardhi kupoteza mbolea yake ya asili siku hadi siku kupelekea mazingira kuharibika huku uzalishaji ukipungua kwa kiasi kikubwa hivyo mdaahalo huo utaibua taswira chanya kwa namna bora ya kilimo chenye tija kisicholeta athari kwa mazingira na afya kwa Wanadamu.

No comments