TLP WATAJA MASHARTI HILI KUSHIRIKIANA UCHAGUZI 2025
Dar es salaam - Chama cha Tanzania labour Party (TLP) kimesema hakiko tayali kushirikiana na chama chochote cha siasa katika uchaguzi mkuu ujao unatarajiwa kufanyika mwezi oktoba 2025 kutokana na kutonufaika na ushiriki wa chama mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho Taifa bwana Richard Lyimo katika mahojiano maalumu na mtandao huu juu ya ushiriki wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa Udiwani, Ubunge na Urais, makao ya chama hicho jijini Dar es salaam.
Bw. Lyimo amesema msimamo huo wa chama ni kutokana na yaliyojili mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 kupitia muungano wa vyama wa Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) ambao vyama viliunganisha nguvu na kutumia rasilimali zao kupiga kampeni kupitia umoja huo lakini mara baada ya uchaguzi havikuweza kunufaika na matokeo ya kura zilizopatikana za Urais na ubunge.
"Mtakumbuka katika uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo vyama viliungana kupitia UKAWA vyama washirika wa muungano huyo vilijiandaa kwa kutumia mpaka rasilimali zake kupiga kampeni katika uchaguzi huo lakini mwisho wa siku wanufaika wakubwa ni chama kilichosimamisha mgombea wa Urais pekee". Alisema Bwana Lyimo.
Alisema mara Baada ya kumalizika kwa uchaguzi chama kilichosimamsha mgombea wa nafasi ya Urais kinanufaika moja kwa moja na kura hizo kwa kupata fursa ya kuteua wabunge viti maalum pamoja kupata ruzuku kitu ambacho vyama washirika awawezi kupata pamoja na ushiriki wao wa hali na mali katika kipindi chote cha kampeni.
Aidha Bwana Lyimo aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo chama cha TLP kimejipanga kushiriki katika chuguzi wa mwaka huu kwa kuhakikisha kuwa kinasimamisha wagombea wenye sifa na mvuto katika ngazi zote kuanzia Udiwani, ubunge na Urais pamoja na kufanya kampeni nchi nzima.
"TLP tumejipanga kwa kuhakikisha kuwa tunateua wagombea wenye ushawishi na mvuto katika ngazi zote sambamba na kuendesha kampeni za kuwanadi wagombea hao na kuwaombea kura nchi nzima kuliko kuingia katika ushirikiano na vyama vingine usiokuwa na tija jambo ambalo linapelekea kuzuia malengo ya chama kupata wawakilishi bungeni pamoja na kushika dola". Alisema Bw. Lyimo.
Akijibu swali juu ya mtizamo wa chama hicho juu ya namna ambavyo inapaswa kuwa hili kiweze kuingia katika ushirikiano na vyama vingine hususani katika uchaguzi wa mwaka huu Bw. Lyimo amesema kama kuna chochote kinaona umuhimu na kuwa na nia ya dhati kushirikiana na TLP basi kiwe au viwe tayali kukubali mgombea atakayepitishwa na chama hicho katika nafasi ya Urais ndio awe mgombea atakepeperusha bendera ya vyama washirika.
"TLP ipo tayali kushirikiana na chama au muungano wa vyama wowote kwa sharti moja tu mgombea atakayepitishwa na chama katika nafasi ya Urais basi ndio awe mgombea katika muungano huo katika uchaguzi mkuu". Alisema Bw. Lyimo
Post Comment