Breaking News

Rc MAKONDA Atoa Ufadhili Wa Matibabu Ya Upasuaji Wa Moyo Kwa Watoto 60 Kutoka Familia Zisizojiweza

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 22 ametimiza ahadi ya kutoa ufadhili wa matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto 10 kati ya 60 alioahidi kugharamia matibabu yao hadi pale watakapopona.

Mhe Makonda alisema ameamua kutoa ufadhili wa watoto 10 kila mwezi kwa kipindi cha miezi sita ambapo zoezi la upasuaji kwa watoto hao litaanza rasmi siku ya Jumatatu ya Juni24 kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea hundi ya Shilingi Milioni 10 kutoka taasisi ya Patel Samaj kwaajili ya matibabu ya watoto 10 kati ya 60 kutoka mikoa mbalimbali mhe Makonda alisema walengwa ni watoto wanaotoka kwenye familia maskini ambazo zimepoteza matumaini kutokana na ukubwa wa garama za matibabu ambapo inaelezwa gharama ya upasuaji ni kwa mtoto mmoja ni kati ya Shilingi Milioni 8 hadi 10.
Aidha mhe Makonda ameipongeza Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa na nzuri ya kutoa huduma za kisasa kwa wagonjwa jambo lililosaidia kuokoa gharama zilizokuwa zikitumika kusafirisha wagonjwa nje ya nchi.

Hata hivyo mhe Makonda ameishukuru taasisi ya Patel Samaj kwa kumuunga mkono kupitia ufadhili matibabu kwa watoto hao ambapo ameziasa taasisi, makampuni na watu binafsi kusaidia matibabu kwa wenye uhitaji.

Kwa upande wao wazazi wa watoto waliopata ufadhili huo kutoka mikoa mbalimbali wamemshukuru mhe Makonda ambapo wameeleza kuwa kwa muda mrefu wamehangahika kutafuta pesa ya matibabu kwa watoto wao bila mafanikio kutokana na ukubwa wa garama.




No comments