Profesa Lipumba: Kazi Ya Jeshi ni Kulinda Mipaka Ya Nchi Si Kununua Korosho
MWENYEKITI wa Chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema serikali ilifanya makosa kwa kulitumia jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenda kusimamiza unuuaji wa Korosho wakati ilitakiwa kutumia sekta binafsi katika kununua zao hilo.
Akizungumza Jijini Dar es salaam wakati akifungua kongomano kubwa la Chama hicho lilofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo kongamano hilo lilopewa jina la “Sauti ya haki na furaha kwa wote”
Profesa Lipumba alisema serikali ilitakiwa kuitumia sekta binafsi katika kununua korosho ili iweze kuinua uchumi wa nchini badala kulitumia jeshi ambapo amedai kazi jeshi ni kulinda raia sio kununua korosho.
“Kuna mambo ambayo sekta binafsi wanaweza kufanya,huna haja ya kupeleka jeshi kwenye korosho,mtu anayekutakia mema ni Yule anayekwambia ukweli, kazi ya Jeshi ni kulinda mipaka ya nchi sio kwenda kununua korosho, tulifanya makosa” Alisema Profesa Lipumba.
Msomi huyo wa masuala ya uchumi amesema kwa sasa hali ya uchumi ni mbaya baada ya kila kona malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai maisha magumu.
“Kwenye ukuaji wa Uchumi katika sekta Binafsi kumekuwa na hali mbaya, mazingira ya kufanya biashara nchini ni magumu, huku mtaani maisha yamekuwa magumu, vijana hawana ajira yote haya yanaonesha kuna shida kwenye uchumi” Alisema.
No comments