Breaking News

MKUU WA MAJESHI ISRAEL KUJIUZULU KWA KUSHINDWA KUZUIA SHAMBULIO

Mkuu wa jeshi la Israel amejiuzulu, kufuatia mapungufu ya kiusalama yaliyosababisha kuuawa kwa watu 1,200 katika shambulizi la Oktoba saba mwaka 2023 lililofanywa na wanamgambo wa Hamas nchini Israel.

Katika barua kwa waziri wa ulinzi, Lt Jenerali Herzi Halevi alikiri kuwa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) "limeshindwa katika dhamira yake ya kuwalinda raia wa Israel".

Jenerali huyo amesema ataacha kazi mwezi Machi wakati wa "mafanikio makubwa" kwa IDF, ingawa alikiri kuwa "sio malengo yote" ya vita ya Israel yamefikiwa.

No comments