NEC Yakutana Na Wawakilishi Wa Wanawake, Watu Wenye Ulemavu Na Vijana.
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi leo imekutana na wawakilishi wa wanawake, watu wenye ulemavu na vijana.
Wadau hao wa Tume
walipata nafasi ya kusikiliza namna ambavyo Tume imejipanga kutekeleza zoezi la
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuanza mwenzi
Juai, mwaka huu.
Kwenye majadiliano
baina yao na Wajumbe na watumishi wengine wa Tume, wadau hao waliishukuru Tume
kwa kuona umuhimu wa kuwashirikisha wadau wote kabla ya kuanza kwa zoezi hilo
na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tume kuelimisha na kuhamasisha wananchi
kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
No comments