Rais MAGUFULI Ang’ara Jarida la Forbes.... Aendelea kukubalika Kimataifa
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ameendelea kukubalika kimataifa
baada ya Jarida maarufu Duniani la Forbes kubashiri kwamba ataivusha Tanzania
na kuwa nchi yenye kipato cha kati kupitia ajenda yake ya Tanzania ya viwanda chini
ya mpango wa maendeleo wa 2025.
Katika jarida hilo
la Forbes Afrika la Julai mwaka huu ambalo lilikuwa mahsusi kwaajili ya kelezea
mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano na uongozi wa Rais Magufuli kwa ujumla,
imeelezwa maono yake kama kiongozi wan chi yameifanya Tanzania kupiga
hatua kubwa za maendeleo na inatarajiwa kuwa miongoni mwa nchi chache sana za
Afrika zenye maendeleo yanayoonekana na yanayopatikana kwa muda mfupi.
Kwamujibu wa Jarida
hilo ambalo limemwelezea Rais Magufuli kama Tingatinga katika kusimamia kile
anachokiamini, miongoni mwa mambo makubwa yanayomfanya ang’ae kimataifa ni
pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya standard Gauge SGR, upanuzi wa bandari na
ujenzi wa miundombinu ya barabara zinazounganisha nchi nzima ambazo ni kichocheo
kikubwa cha maendeleo hapa nchini.
Aidha Rais Magufuli
ameelezewa kuwa ni mtu asiye na masihara katika kusimamia masuala ya maendeleo,
mfano jinsi alivyosimamia na kuhakikisha uwanja wa ndege wa Julius
Kambarage Nyerere terminal three unakamilika kwa wakati na kwa kiwango cha
kimataifa.
Jarida la Forbes
limeendelea kumwelezea Rais Magufuli kuwa, mafanikio mengi anayopata ni
kutokana na kuongozwa na mpango wa maendeleo wa 2025 pamoja na ilani ya
Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015.
Miradi mingine
iliyoainishwa kuonyesha utendaji wake ni ile ya umeme ya Kinyerezi awamu
ya kwanza ya pili nay a tatu, pamoja na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika
maporomoko yam to Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge,ambayo lengo lake ni
kumaliza kabisa tatizo la umeme hapa nchini hasa kwa wananchi wa vijijini.
Kuhusu ukuaji wa
uchumi Jarida la Forbes limeelezea kuwa katika kipindi cha utawala wake tangu
aingie madarakani mwaka 2015, uchumi umeendelea kukua kwa kasi kwa kiwango cha
asilimia 7 ambao ni ukuaji wa mfano na wakuridhisha kwa nchi za
Afrika ikilinganishwa na miaka mingi iliyopita.
Katika uwekezaji
Rais Magufuli amenukuliwa akiwahakikishia wawekezaji na dunia kwa ujumla
kwamba, Tanzania ni nchi salama na kwa uwekezaji na akawakaribisha kuja kuwekeza
kwani ameendelea kufanya mapinduzi makubwa katika uwekezaji lengo kuu ikiwa ni
kuvutia wawekezaji wengi zaidi.
Mahojiano ya Rais
Magufuli yaliyotolewa na Jarida la Forbes Africa, yalifanyika mapema
mwaka huu ambapo Jarida hilo lilikuwa na toleo maalum la Tanzania kuhusiana na
mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali.
Credit: Michuzi
No comments