NEC Yakutana Na Wahariri Wa Vyombo Vya Habari, Waandishi Wa Habari Na Waandishi Wa Makala.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage akizungumza katika ufunguzi wa mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari, Waandishi wa habari na Waandishi wa makala.
Dar es salaam;
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi leo imekutana na Wahariri wa vyombo vya habari, Waandishi wa habari na
Waandishi wa makala.
Akizungumza kwenye
mkutano huo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa
Semistocles Kaijage amesema wanahabari ni wadau muhimu sana wa Tume kwa kuwa
wao ndio wanaiunganisha Tume na jamii.
Mkutano huo
umefanyika ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura unaotarajiwa kufanyika mwenzi Julai, mwaka huu.
Mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), Athumani kihamia akiongea katika ufunguzi wa mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari, Waandishi wa habari na Waandishi wa makala.
Baadhi ya Wahariri
Na Waandishi wa makala kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifatilia
madazilizokuwa zikiwakilishwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage akifafanua jambo katika mkutano huo.
Wandishi kutoka vyombo
mbalimbali ya habari wakichukua matukio katika mkuutano huo.
Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage katika picha ya pamoja na wahariri na waandishi wa makala kutoka vyombo
mbalimbali vya habari.
No comments