Rais MAGUFULI Anakubalika Kwa Asilimia 91 Kwa Mujibu Wa Matokeo Ya Utafiti
Utafiti ulifanywa
na kampuni tatu nchini uoyesha kuwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Mhe. John Pombe Magufuli umeonyesha kuwa asilimia 91 ya wananchi walihojiwa
katika utafiti huo wameelezea kuridhishwa na utendaji na hatua mbalimbali anazochukua
tangu aingie madarakani.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwanaharakati Huru na Mkurugenzi wa
kampuni ya CZ Media Bw. Cyprian Musiba alisema utafiti huo ulihusisha watu
wenye umri wa miaka 18 hadi 45 na miaka 45 hadi 75 ulijikita zaidi katika
maeneo makuu manne ambayo Maendeleo, Utawala bora, Elimu, Afya na utendaji wake
kwa ujumla wake.
“Katika Utafiti huu
wananchi waliohojiwa asilimia 91 walisema wanalidhishwa na namna Rais Magufuli
anavyo ongoza kwa kusimamia asilimali za nchi wakati asilimia 9 walisema
asimamii ipaswavyo kutokana na kupewa taarifa zisizo sahihi zinazohusu miradi ya maendeleo” alisema bw. Musiba.
Alisema kwa mujibu
wa utafiti huo wananchi pia wameonyesha kuwa na imani kwa asilimia 81 na Rais
Magufuli kuwa anaweza kutatua kero zote za watanzania katika mda wake ulibakia wa
kuwepo madarakani wakati asilimia 17 wao walisema hatofanikiwa kumaliza kero
hizo wakati asilimia 2 ya wananchi walioulizwa walisema wajui chochote.
“Vijana ambao
waliojiwa wenye umri wa miaka 15 hadi 45 ambao ni wanafunzi wa kuanzia kidato
cha sita na vyuo chuo kikuu kwa njia ya simu na uso kwa uso katika nyanja ya
elimu asilimia 62 walisema wanaridhishwa na jitihada anazochukua rasi Magufui hususani
kwa hatua yake ya kutoa elimu bure, ujenzi wa maktaba ujenzi wa hosteli, wakati
asilimia 20 wakisema waridhishwi wakati asilimia 3 wao walisema awajuhi”
alisema.
Aidha bw Musiba
aliongeza kuwa kwa upande wa walihojiwa katika utafiti huo wenye miaka 45 hadi 75
kuhusu wanaamini kama rais Magufuli atashinda urais katika uchaguzi ujao
asilimia 89.9 waliesema atashinda kutokana na namna katika awamu yaje ya kwanza
alivyojikita zaidi katika kutatua kero za wananchi na jitihada ambazo amekuwa
akizchukua katika kuwaletea maendeleo wananchi, wakati asilimia 19.1 wakisema hawezi
kushinda wakati watanzania wanaoishi nje ya nchi waowakisema atashinds kwa
aslimia 83wakati aslimia 17 wakisema hatoshinda.
Utafiti huo
umefanyika katika mikoa ya Mwanza, Dar es salaam, Arusha, Kigoma, Pwani,
Kilimanjaro, Dodoma, Mara, Rukwa, Ruvuma, Simiyu, Unguja na Wete, Pemba, Norway
na Uibgereza.
No comments