Breaking News

PROFESA IBRAHIM LIPUMBA AFANYA UTEUZI WA WAKURUGENZI, MAKATIBU, HAYA HAPA MAJINA YA WALIOTEULIWA

Kwa kuzingatia Ibara ya 94(1)(f) ya Katiba ya CUF- Chama Cha Wananchi ya mwaka 1992 Toleo la mwaka 2019, Mwenyekiti wa Chama Taifa amepewa Mamlaka ya kuteuwa Wakurugenzi, Manaibu Wakurugenzi, Katibu na Naibu Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibiti baada ya kushauriana na Makamu Wenyeviti.

Wafuatao wameteuliwa kushika nafasi zilizoainishwa kwenye Ibara iliyotajwa hapo juu:-

1. Rajab Mbarouk Mohamed- Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibiti;
2. Juma Wandwi - Naibu Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibiti;
3. Eng. Mohamed Ngulangwa- Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma;
4. Ali Rashid Ali (Abarani)- Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma;
5. Amina Ali Hamad - Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria;
6. Rashid Mweyo- Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria;
7. Zaynab Amir Mndolwa - Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi;
8. Nawiya Abdallah - Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi;
9. Hamis Hamad Ibrahim - Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi;
10. Yusuf Mbungiro - Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi;
11. Mneke Jafar- Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge, Sera na Utafiti.
12. Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge, Sera na Utafiti atatangazwa baadae.

Wakurugenzi wateule wanaanza kazi mara moja na Uteuzi huu utafikishwa kwenye Kikao kijacho cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa ajili ya kuthibitishwa

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!

Prof. Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti Taifa
CUF- Chama Cha Wananchi
Januari 20, 2025```
 

No comments