Breaking News

WAWILI MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMUUA NDUGU YAO KISHA KUMZIKA

Dar es salaam - Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili Fredy Rajab Chaula na Bashiru Richard Chaula kwa tuhuma za kula njama ya mauaji ya Regina Rajab Chaula (62) mkazi wa Bahari Beach Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambaye ana makazi mengine nchini Denmark.

Akizungumza tukio hilo mapema leo January 20,2025 jijini Dar es salaam Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema mauaji hayo yametokea wakati mama huyo akiwa kwenye harakati za kufuatilia kesi zake za madai dhidi ya watuhumiwa hao, ambazo ziko Mahakama Kuu Divisheni ya ardhi jijini Dar es Salaam.

Alisema mwili wa mama huyo ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Desemba 13, 2024, umepatikana Januari 18, 2025, majira ya saa 8 mchana ndani ya nyumba yake.

“Wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa kupotea kwa mama huyo, lilibaini na kutilia mashaka shimo kubwa la maji machafu lililojengewa katika nyumba yake, ambapo lililazimika kulibomoa na kuukuta mwili wa marehemu”. Alisema kamanda Muliro 

Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi linalaani vikali kitendo hiko kibaya na cha kinyama alichofanyiwa mama huyo, na litahakikisha kila aliyekula njama ama kushiriki kwa namna yoyote anakamatwa na kufikishwa kwenye mamlaka za kisheria.

No comments