MKUTANO MKUU CCM WAAZIMIA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KUWA MGOMBEA URAIS 2025
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 19 Januari, 2025.
Dodoma - Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo tarehe 9 Januari 2025, kwa kauli moja wamepitisha azimio la Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kuwa mgombea urais atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao 2025
Akisoma azimio hilo amesema “wajumbe wa mkutano mkuu tumeazimia`Kumteua Mwenyekiti Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.“`
Azimio hili limepitishwa na wajumbe 1978 wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi bila kuathiri katiba ya chama cha Mapinduzi.
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Mkutano Mkuu una mamlaka ya kufanya maamuzi haya. Kulingana na Katiba ya CCM, Ibara ya 8(2)(a) inasema:-
”Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi una mamlaka ya kumteua mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.”
No comments