Kongamano La Kuliombea Taifa Kufanyika 30 June Jijini Dar Es Salaam.
Watanzania wametakiwa kuendelea kuliombea taifa ili liweze kuendelea kuwa kisiwa cha amani
na utulivu pamoja na kuepuka viashiria vyote vya uvunjifu wa amani na umoja
tulio nao tangu kuasisiwa kwa taifa letu.
Akizungumza Jijini
Dar es Salaam na Kiongozi wa Kanisa la Redeemed Gospel Church Miracle Center (RGCM),
Dkt. Peter Nyaga katika Ibada maalumu ya kuliombea Taifa Amani kuelekea uchaguzi
wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwake huu.
“Taifa linapokuwa
na amani, umoja na utulivu bila ya kuwa na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa
amani, umoja na mshikamano uliopo litaendelea kusonga mbele na Mungu atazidi
kulibaliki” . Alisema Dr Nyaga.
Alisema katika kuhakikisiha
taifa linaendelea kuwa na amani, umoja ulipo atafanya maombi ya kumwombea Rais
John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wote wa serikali ili wawe na nguvu ya
kuendelea kuliongoza taifa vizuri.
“Katika kuhakikisha
taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu nimepanga kuandaa kongamano maalum
la kuliombea taifa lizidi kuwa na amani litakalofanyika tarehe 30 mwezi huu
katika viwanja vya shule ya Msingi Tabata Liwiti” alisema Dkt. Nyaga.
Akizunguzia katazo
la serikali juu ya matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kiongozi huyo wa kiroho
alisema Kanisa linaungana na serikali kupiga marufuku mifuko hiyo ya plastiki nchini.
“Tunaungana na
serikali kuhusu kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki nchini natoa wito kwa
wahumini kuunga mkono swala hilo kwa kutumia mifuko mbadala hili kulinda na
kutunza mazingira” Alisema Dkt. Nyaga.
Baadhi ya waumini
wakiendelea na maombi.
No comments