Katibu Mkuu Chama Cha FRELIMO Roquel Silva, Vijana Wana Jukumu La Kuongoza Mapambano Ya Kulikomboa Bara La Afrika Kiuchumi.
Na: Elisa Shunda, Bagamoyo.
RAI imetolewa kwa vijana wa kiafrika kushirikiana kwa pamoja katika kuongoza jukumu la mapambano dhidi ya wakoloni mamboleo katika kuyakomboa mataifa yao na afrika kiuchumi.
RAI imetolewa kwa vijana wa kiafrika kushirikiana kwa pamoja katika kuongoza jukumu la mapambano dhidi ya wakoloni mamboleo katika kuyakomboa mataifa yao na afrika kiuchumi.
Hayo yamesemwa na
Katibu Mkuu wa Chama Cha Frelimo, Roquel Silva Samuel leo wakati alipotembelea na kuangalia historia ya eneo
ambalo lilikuwa hifadhi ya Rais wa Kwanza wa Nchi ya Msumbiji,Samola Machel
eneo la Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole ambapo yeye na wasaidizi wake
wameweza kuona nyumba aliyoishi mkombozi huyo wa nchi ya Msumbiji na
Wenzake,Bwalo la Chakula,Darasa la Mafunzo Mbalimbali na Mbinu za Kivita na
Eneo Ambalo kulikuwa na handaki kwa ajili ya uhifadhi wa silaha zao.
''Vijana wa
Kiafrika wa zamani akiwemo Rais wa Kwanza wa Msumbiji,Samora Machel waliweza
kutumia ujana wao katika ukombozi wa nchi zao hata hata hayati mwalimu Julius
Nyerere alianza harakati za ukombozi wa Tanganyika akiwa na umri wa kijana, kwa
sasa vijana wa sasa wengi wao ujana wao wanaamini wanautumia vizuri ujana wao
baada ya kuona tayari labda washapata kununua usafiri kama pikipiki,gari au
nyumba ya kuishi wanaona tayari wameshajikomboa kimaisha.
''Mimi nasema
hapana vijana wa kiafrika mnapaswa kushirikiana kwa pamoja katika kuongoza
jukumu la mapambano dhidi ya wakoloni mamboleo katika kuyakomboa mataifa yenu
katika bara letu la afrika kiuchumi kwa kuwa hawa wanyonyaji na wakoloni
wanatunyonya mali zetu katika njia ambazo sisi tunachekelea kumbe ndo
wanatuumiza taratibu nchi zao za ulaya zinaneemeka wanaishi kwa raha mustarehe
ila utajiri wote wanachukua kwetu afrika nawasihi vijana mbadilike muwe kitu
kimoja katika vita hii'' Alisema Katibu Samuel.
Aidha katibu huyo
mkuu wa chama cha Frelimo baada ya kutembelea nyumba aliyokuwa akiishi mpigania
uhuru wa nchi yao Hayati Samora Machel na Wenzake pamoja na sehemu zingine
alisema kuwa chama chake kitashirikiana na chama cha mapinduzi (CCM) katika
kuhakikisha wanarekebisha nyumba hiyo pamoja na kuhakikisha sehemu hizo muhimu
katika historia ya nchi yao inabaki kuhifadhiwa ili iwe ukumbusho na utalii kwa
wananchi wa Nchi ya Msumbiji,Ulimwenguni na vizazi vijavyo wajue umuhimu na
undugu wa kweli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nchi ya Msumbiji.
Akiongea katika
ziara hiyo,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Bashiru Ally Kakurwa
alisema kuwa vita hiyo si vita ya silaha na bunduki bali ni vita ya mshikamano
ni lazima wajenge umoja kwanza na akasema wameingia katika mfumo wa vyama vingi
lakini bado vyama hivyo havijaisaidia katika kujenga mshikamano wa
kitaifa,kimataifa katika Afrika na nchi zote maskini,funzo hatuwezi kushinda
vita hiyo bila kuwa na umoja wa kitaifa na umoja wa afrika.
''kazi ambayo
hatujafanya sisi kizazi cha sasa ni kuiunganisha afrika ili nchi za bara hilo
zifanye biashara,uwekezaji,ziendeshe mashule,tafiti kuhusu kilimo kwa pamoja
hatujafika huko,lakini sisi Tanzania tumeanza kuonyesha njia tumefufua shirika
letu la ndege na sasa hivi linafanya safari Zimbabwe,Afrika Kusini na baadae
nchi zingine,katika ziara ya hivi karibuni ya Rais Dk.John Pombe Joseph
Magufuli tumepata masoko ya mahindi katika nchi za Namibia na Zimbabwe.
''Sisi Tanzania
kupitia chama chetu cha CCM tumezidi kuweka mahusiano mazuri leo hii Frelimo ya
Msumbiji,Swapo ya Namibia,ANC ya Afrika Kusini,MPRA ya Angola na ZANUPF ya
Zimbawe vyama sita tunajenga kwa pamoja Chuo cha Uongozi na Siasa cha kisasa
pale Kibaha ili vijana na makada wa vyama hivi wajifunze namna vijana wenzao
waliopita walivyoshiriki katika mapambano ya ukombozi ndio maana leo pia ugeni
huu tulipitia katika eneo hilo linalojengwa chuo hicho'' Alisema Katibu Mkuu
CCM Taifa,Bashiru Ally.
Pia Katibu Bashiru
ametoa siku tano kwa uongozi wa Mkoa na Chama Pwani kuleta mpango jinsi
ukarabati wa chuo cha mifugo na kilimo kwa sasa ambapo awali Rais wa
Zimbabwe,Emerson Mnangagwa alisoma katika chuo hicho kama mpigania uhuru
aliacha mchango wa Dola Elfu Sitini ili zisaidie kukarabati sehemu ya majengo
ya chuo hicho.
Alisema ni mwaka
mmoja sasa bado hajaletewa amemuagiza mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhandisi Evalist
Ndikilo kuhakikisha mpango mkakati wa ukarabati wa jengo hilo na upimaji wa
ardhi ya eneo hilo unakamilika ili zoezi la ukarabati uanze mara moja.
Mkutano Huo
Umehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Abdallah Haji
Haidari,Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Taifa,Erasto Sima,Katibu Jumuiya ya Wazazi
Pwani, Gama Juma Gama, Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Wilay ya Bagamoyo, Abubakar
Mlawa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kibaha Mjini, Edwin Shunda, DC Bagamoyo, Zainab Kawawa, Mbunge
Chalinze, Ridhiwan Kikwete
No comments