Breaking News

Dkt. Bashiru Mgeni Rasmi Uzinduzi Wa The Capt Komba Arts Memoris Foundation utakaofanyika 6, Julai Jijini Dar


Katibu wa chama cha mapinduzi dokta Bashiru Ally anategemewa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya The Capt Komba Arts Memoris Foundation utakaofanyika tarehe 6 julai katika ukumbi wa kijiji cha makumbusho ya taifa kijitonyma jijini dar es salaam.

Akuzungumza mapema jijini dar es salaam mratibu wa uzinduzi huo Bi salome Komba ambaye ni mjane wa maerehemu komba alisema lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kumuenzi na kuendeleza mchango mkubwa wa marehemu komba katika kipindi chote cha uhai wake.

"lengo la kuanzishwa taasisi hii ni kuakikisha tunaenzi na kuendeleza mchango wa maheremu katika nyanja mbalimbali hususani Siasa, sanaa na Maswala ya kijamii" Alisema Bi Salome.

Alisema sambamba na uzinduzi huo pia taasisi hiyo itaanzisha band itakayo tambulika kwa jina la The Capt Komba Memorial Band (CKM Band) ambayo itaundwa na vijana ambao watapatikana kuwa kufanyiwa usaili ambao utafanyika tarehe 22 na 23 katika ukumbi wa idara ya Sanaa ndani ya chuo kikuu cha dra es salaam (UDSM).

"Katika kuenzi kazi alizofanya marehemu komba taasisi itaanzisha pia band ambayo itaundwa na vijana wenye vipaji vya kuimba sauti kama ya marehemu ambao watafanyiwa usaili na na jopo la majaji sita waliobobea katika fani ya sanaa" Alisema Bi Salome
Mapema katibu wa Taasisi hiyo Bi Catheline Kahabi akielezea namna viajana hao ambao wataunda band hiyo watakavyopatikana, kutakuwepo na mchujo na ambao awakuweza kufika lakini wangependa kushiriki badae watatangaza namba ya wasap na email ambazo zitatumika kuwasilisha kazi zao kwa kujirekodi video na kutuma.

"Vijana ambao watataka kushiriki katika usaili huu kutakuwa na vigezo ambavyo mshiriki anataliwa kuwa na miaka 18 mpaka 25, Mshiriki atajaza fomu maalum ambazo zitatolewa bure chuo kikuu cha dare s salaam na nyumbani kwa marehumu mbezi beach tangi bovu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa band ya TOT bw. Gasper Tumaini alisema marehemu alikuwa na mchango mkubwa sana hususani katika sanaa ambapo kazi zake zote zimekuwa zikitumika katika kipindi karibu cha awamu zote za uongozi tangu nchi ipate uhuru.

Alisema wao kama TOT band watashirikiana na taasisi hiyo kukhakikisha inafikia malemgo yake na kuwataka washiriki ambao watakuwa wanataka kushiriki na awana nyimbo za marehemu za kufanyia mazoezi kufika ofisini kwao mwannyamala kwa mwinyi Juma jijini dar es salaam kuweza kupatiwa nyimbo hizo.

No comments