Waziri Mkuu: Tutumie Siku Ya Eid Kwa Kutenda Mema
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waislamu wote nchini watumie siku kuu
ya Eid el Fitr kwa kutenda matendo mema pamoja na kuwakumbuka yatima na
wajane.
“Leo
ni siku kubwa na muhimu waislamu wanahitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu
wa Ramadhani na kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, hivyo tuendeleze
matendo mema.”
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 5, 2019) wakati aliposhiriki
swala ya Eid El Fitr katika msikiti wa Anwar uliopo Msasani jinini Dar
es Salaam.
Waziri
Mkuu amesema wakati huu ni mzuri kwa kuimarisha mshikamano miongoni
mwenu na madhehebu mengine, hivyo hakikisheni mnayaendeleza mambo mema
yote.
“Tumeona
utulivu uliojitokeza katika mwezi mtukufu, na jambo hili limesisitizwa
na viongozi wa dini. Tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikamano na
tuvumiliane.”
Pia,
Waziri Mkuu amewakumbusha wazazi na walezi kuwaongoza watoto kwa kuwapa
mafundisho ya dini yatakayowawezesha kumjua Mwenyezi Mungu na kuwa raia
wema.
Awali,
Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mhina alisema waislamu wanatakiwa kuitumia
siku ya leo kwa kuhamasisha Amani pamoja na kuwasaidia watu wasiokuwa
na uwezo.
Pia
amewasisitiza wayaendeleze mema yote waliyoyafanya katika kipindi cha
mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu na kuwajali
wazazi wao.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
No comments