Breaking News

MOI Yapokea Msaada Wa Miguu Bandia 600 Kutoka Ubalozi Wa India


Waziri wa afya mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi mguu bandia kwa mmoja wa muhitaji katika hafla ya utoaji wa vifaa tiba hivyo kwa watu wenye ulemavu iliyofanyika katika Taasisi ya Mifupa (MOI), wa kwanza kulia Mkurugenzi wa MOI, dkt. Respicious Boniface, koshoto kwake ni balozi wa India nchini Sandeep Arya.
Waziri wa afya, maendeleo ya Jamii, Wazee na watoto mhe. Ummy Mwalimu akifafanua jambo katika hafla hiyo.

Dar es salaam:
Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, wazee na watoto kwa kushirikiana na ubalozi wa India nchini kupitia taasisi ya utengenezaji wa Viungo bandia ya (BMVSS) imetoa msaada wa miguu ya bandia zaidi ya 600 kwa watu wenye ulemavu wa miguu nchini.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa miguu hiyo ambayo imefanyika katika taasisi ya mifupa (MOI), Waziri wa afya, maendeleo ya Jamii, Wazee na watoto mhe. Ummy Mwalimu alisema deriakali inatambua uwepo wa changamoto ya upungufu wa miguu bandia kwa ajili ya watu wenye ulemavu tayali imeshaanza chukua hatua za kuhakikisha wale wote wenye uhitaji wa miguu hiyo wanapatiwa.

"Tulitangaza kwa wale wote wenye uhitaji wa miguu bandia kujiandikisha kuomba ambapo jumla ya watu 500 ndio tulikuwa tumelenga,lakini waliojitokeza kuomba ni 900 na jumla ya miguu bandia iliyopatikana ni 600 hivyo watu 300 awataweza kupata, lakini nikiwa kama waziri mwenye dhamana   ya afya nitahakikisha na kuangalia namna ili kuwezesha wahitaji hao 300 kuweza kupata miguu hiyo" Alisema Mhe. Ummy.

Alisema pamoja na jitihada za serikali katika kuhakikisha inaboresha upatikanaji wa huduma na miundombinu bado kumekuwepo na changamoto kubwa ya kuwepo kwa ajali za barabarani jambo ambalo ni chanzo kikubwa kinachosababisha kupoteza viungo kwa kusababisha ulemavu jambo ambalo linapelekea kusababisha kurudisha nyuma maendeleo ya waathirika pamoja na taifa kwa ujumla.
"Kwa mujibu wa takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa hospitali za wilaya, hosptali za Rufaa za mikoa wamekuwa wakipokea idadi kubwa ya wagonjwa wanaotokana na ajali zinazosababoshwa na ajali, ambapo mwaka 2014 wagonjwa 200 hadi 300 walikuwa wanapokelewa lakini kwa sasa takwimu zinaonyesha kuwa wagonjwa wanaopokelewa kutokana na ajali ni 500 mpaka 600." Alisema.

Aidha mhe Ummy aliongeza kuwa kutokana na hali ilivyo kwa sasa serikali ina mpango wa kupeleka muswada bungeni kuhakikisha moja ya masharti kwa madereva wa bodaboda wazima wawe wanamiliki bima ya afya ili kuwahakikishia matibabu wapatapo ajali.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya mifupa (MOI), Dkt. Respicious Boniface alipongeza serikali ya awamu ya tano kwa inayoongozwa na rais Magufuli kwa jitihada ambazo imekuwa ikizichukua kuiwezesha taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma bora zaidi.

"Nitoe pongezi kwa serikali kwa hatua ambazo imekuwa ikizichukua katika kuakikisha taasisi hiyo inaendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi, ikiwemo kutoa fedha za kununua vifaa vya kisasa jambo ambalo limesaidia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa wagonjwa ambao wangeenda kufata matibabu nje ya nchi". Alisema dkt. Boniface

No comments