MFANYABIASHARA JOE KARIUKI AMUANGUKIA RAIS MAGUFULI
Pichani bw. Joe Kariuki ambae pia aliwahi kuwa meneja wa Mr Nice chini ya Label yake ya Candy N' Candy Records nchini Kenya.
Mkurugenzi wa kampuni ya Candy N' Candy ya nchini Kenya na wazalishaji wa jarida la Babkubwa la hapa Tanzania Joe Kariuki ameshukuru uongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa kutenda haki hadi kuachiliwa huru ambapo alikuwa akikabiliwa na kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Amesema hayo wakati akifanya mahojiano na vyombo vya habari akiwa jijini Nairobi Kenya ambapo amesema anaishukuru mahakama ya Arusha kutenda haki hadi kuachiliwa huru ambapo aliweza kukaa gerezani kwa takribani mwaka mmoja tangu alipohukumiwa kisha kushinda rufaa yake.
"Kwa kweli naishukuru mahakama ya Arusha kwa kuweza kutenda haki hadi mimi kuachiwa huru kwa kushinda rufaa hii imedhihirisha kwamba serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imekuwa ikisimamia haki katika vyombo vyake kwa kusikilizwa kesi kwa hharaka zaidi na kutoa haki" amesema Joe Kariuki.
Aidha amewashukuru Watanzania wote na wafanyakazi aliokuwa akifanya nao kazi kipindi akiwa hapa nchini na kusema muda si mrefu angependa kurudi Tanzania na kuendelea kuwekeza katika sekta mbalimbali na kutoa ajira kwa watanzania.
"Nipende kuwashukuru watu niliokuwa nikifanya nao kazi na watanzaia wote kwa kuniombea na kuwa nami katika kipindi hiki kigumu nilichopitia nami nawaahidi ningependa kurudi Tanzania na kuendelea kuwekeza katika sekta mbalimbali hivyo bado tupo pamoja" ameongeza Kariuki.
Hata hivyo baada ya kuachiliwa huru kwa kushinda rufaa mfanyabiashara huyo amerudi nyumbani kwake Nairobi, Kenya kwa ajili ya mapumziko kabla ya kurejea nchini kuendelea na biashara zake ambazo zilisimama kwa muda kipindi akiwa gerezani.
Joe Kariuki alikamatwa Namanga wilaya ya Longido mnamo tarehe 2 mwezi Julai na kufikishwa mahakama ya wilaya ya Longido na kufunguliwa mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa mfanyabiashara mwenzake Yusuf Mohamed na mwaka jana 2018 kuhukumiwa kwenda jela miaka 7 kabla ya kushinda rufaa yake na kuachiwa huru tarehe 10 mwezi Mei 2019 na mahakama ya Arusha.
No comments