Breaking News

Manispaa Ya UBUNGO Yazindua Rasmi Magari Matatu

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imezindua rasmi magari matatu ambayo ni gari maalum kwa ajili ya maji taka SM 12769, Mazda Tribute SM 12717 na Mazda Bongo SM 12716 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya ofisi.

Uzinduzi huo umefanyika leo katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo makao makuu Kibamba CCM na Kuhudhuliwa na wakuu wa Idara na vitengo wa Manispaa hiyo.

Akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo  kwa ajili ya Uzinduzi wa magari hayo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Beatrice R. Dominic alisema Manispaa tulitenga bajeti na kufanikiwa kununua gari la maji taka kwa Tsh Milioni 272 na magari mengine mawili tumeyapata kwa wadau kutokana na mahusiano mazuri.
Gari moja ndogo litatumiwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii na nyingine itatumika katika shughuli za mapato na matumizi mengine ya kiofisi katika Manispaa yetu hivyo Mkuu wetu wa wilaya tunakukaribisha kufungua magari haya.

Baada ya kukaribishwa kwa ajili ya ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare makori amepongeza ununuzi wa gari kubwa la kunyonya maji taka kwa kuwa litasaidia katika ustawi wa watu wetu wa Ubungo ususani katika suala zima la afya.
Pia amesema kwa kuwa idara ya maendeleo ya jamii imekabidhiwa gari ni matumaini yake kuwa litasaidia katika kurahisisha ufuatiliaji na usimamizi  wa vikundi vya mikopo ya Kinamama na vijana na hivyo kurahisisha utendaji kazi katika idara hiyo.

Wito wangu kwenu mnaoenda kutumia magari hayo hakikisheni yanatunzwa na yatumike katika matumizi lengwa alisisitiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
Aidha amewataka watumishi wote kuendelea kuchapa kazi kwa kuzingatia ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kasi ileile ya Raisi wetu mpendwa Mhe Dkt John Pombe Magufuli ili kuwaletea wananchi Maendeleo. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

No comments