Breaking News

Rais Shein:Ni Muhimu Kufanyika Utafiti Kubaini Faida Zitokanaazo Na Zao La Karafuu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesisitiza azma ya Serikali ya kuendelea  kuwalipa asilimia 80 ya bei ya Karafuu katika soko la Dunia, ili kuwatia moyo wakulima wa zao hilo.

Dk. Shein amesema hayo katika  ukumbi wa Ikulu ndogo Kibweni mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda, wakati ilipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango kazi wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai 2018 hadi Machi, 2019.

Alisema  pamoja na bei ya zao hilo kupanda na kushuka katika soko la Dunia, Serikali itaendelea na utaratibu wake uliodumu kwa miaka minane sasa wa kuwalipa wakulima kiwango hicho, ambapo ni shilingi 14,000/- kwa kilo moja ya daraja la kwanza.

 Pia aliupongeza uongozi wa ZSTC pamoja na watendaji wake kwa utulivu mkubwa unaoliwezesha shirika hilo kupata maendeleo makubwa na kuliendeleza zao hilo.

No comments