Breaking News

Amana Bank Yakabidhi Zawadi Kwa Washindi Wa Shindano La Kuifadhi Quruan 2019

Mkuu wa idara ya masoko wa bank hiyo bw. Dassu Mussa akimkabidhi fedha taslimu million 20 kwa mshindi wa kwanza mashindano ya kuifadhi Qur'an Mouhamed Dialo kutoka nchini Senegal katika hafla iliyofanyika jijini dar es salaam
Mkuu wa idara ya masoko wa bank hiyo bw. Dassu Mussa akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano maalum ya 20 ya kuifadhi Qur'an jijini dar es salaam
katibu wa taasisi ya Al-HIKMA ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo Alhajj Mussa Mushi akifafanua jambo katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano maalum ya 20 ya kuifadhi Qur'an jijini dar es salaam.
Pichani ni Mshindi wa kwanza Mouhamed Dialo (wa kwanza kulia) kutoka nchini Senegal, Mshindi wa pili Faruq Yakoub (katikatiki) kutoka nchini Nigeria, mshindi wa tatu Shamsuddin Hussein (wa kwanza kushoto) kutoka Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiliwa zawadi zao.
Picha ya pamoja.

Dar es salaam.
Bank ya kiislam ya Amana bank imekabidhi zawadi kwa washindi watatu wa mashindano ya 20 ya kuifadhi Qur'aan tukufu mwaka 2019 yaliyofanyika katika uwanja wa taifa na kushuhudiwa na Rais John Pombe Magufuli.

Akizungumza katika halfa ya kuwakabidhi zawadi jijini dar es salaam mkuu wa idara ya masoko wa bank hiyo bw. Dassu Mussa alisema wamekuwa wakisaidia taasisi ya Al-HIKMA foundation ambao ni waandaaji wa mashindano hayo kutokana na kutambua umuhimu wa mashindano hayo katika kuwajenga vijana katika maadili mema.

"Kwa kipindi kirefu tumekuwa tukishiriki kuandaa mashindano haya makubwa zaidi ya kuifadhi Qur'an tukufu afrika ambapo mwaka huu mhe rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi hivyo amana bank leo inawakabidhi washindi zawadi zao." Alisema bw.Mussa.

Alisema leo tunakabidhi zawadi kwa washindi wa kwanza Mouhamed Dialo kutoka nchini Senegal atapokea kiasi cha tsh million 20, Mshindi wa pili Faruq  Yakoub kutoka nchini Naijeria million 12, wakati mshindi wa tatu Shamsuddin Hussein kutoka Zanzibar ambaye amejinyakulia million 7.5.

Mapema akizungumza katika hafla hiyo katibu wa taasisi ya Al-HIKMA ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo Alhajj Mussa Mushi alisema wanatoa shukrani za dhati kwa amana bank kwani wamekuwa wakishiriki kuandaa mashindano hayo kwa kipindi kirefu nchini.

"Taasisi ya Al-HIKMA imekuwa ikiandaa mashindano haya makubwa barani afrika kwa ufadhili wa amana bank kwa kuwezesha kufanyika mashindano haya kwa mafanikio nchini" Alisema bw. Mushi. 

No comments