Breaking News

LHCR Yazindua Ripoti Ya Haki Za Binadamu Kwa Mwaka 2018

Kituo cha sheria na haki za binadamu kimezindua ripoti ya haki za binadamu ya mwaka 2018 ambayo inaonyesha kuwa vitendo vya ukatili wa kingono limekuwa tishio kwa haki na ustawi wa mtoto nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo jijini dar es slaam mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu bi Anna Henga alisema kwa mujibu wa ripoti hiyo inaonyeaha matukio ya ukatili dhidi ya watoto umeongezeka zaidi katika kipindi cha mwaka 2018.

"Kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa ya mwaka 2018 inaonyesha kuwa kumekuwepo na ongezeko la matukio ya ukatili wa kingono kitendo ambacho kipelekea kuwa tishio juu ya ustawi wa haki za mtoto nchini" Alisema bi henga.

Alisema kumekuwepo na changamoto nyingi   mfano uhuru wa kujieleza ambao ni haki ya msingi ya binadamu hususani kwa vyombo vya habari haki ya kupiata habari na uhuru wa kutia maoni imeripotiwa umeendelea kudorora na kuasiri shughuli za asasi za kisiasa, watetezi wa haki za binadamu, vyama vya siasa na uhuru wa kijamii kwa ujumla.
Mapema akielezea namna ripoti hiyo ilivyoandaliwa Afisa utafiti wa Lhcr Bw. Fundikila Wazambi alisema lengo kubwa ninkuelezea hali za haki za binadamu nchini kwa mwaka 2018 kwa kuonyesha ukuaji wa haki na jitihada zanazofanyika kuzilinda.

Alisema taarifa ya kuandaa ripoti hii zimekusanywa kutoka katika taasisi mbalimvali za serikali ikiwemo mahakama, Bunge, Jeshi la polisi, Maafisa kutoka Halmashauri nchini pamoja na waangalizi wa haki za binadamu.

Amezitana haki ambazo zimejunjwa sana kwa mwaka 2018 kwa mujibu wa taarifa ya ripoti hiyo kuwa ni ukali dhidi ya haki hasa za watoto, haki za kuishi, Uhuru wa kujieleza Haki ya kuwa huru na salama pamoja na uhuru wa kujieleza.

Ripoti ya haki ya haki za binadamu ya mwaka 2018 imekusanywa kutoka katika mikoa ya Mwanza, Tabora, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Shinyanga, Singida, kigoma pamoja na Dar es salaam..

No comments