TAMWA Yaendesha Mafunzo Ya Siku Mbili Kwa Waandishi Wa habari
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPFGa1xu5LGTsWnk8vB0z_9X8QQSBIVZPLCLLOo0XLaEuGs1gbS5oY-ffuNJYA4uV8W3XgRD-WJufqbI8-K2hkxecAvTX7_sCgIPZ46O9an_lOlpIieqFHx_JkI2yK18GSzivauY01f9jQ/s640/IMG_20190405_101333%257E2.jpg)
Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) wameandaa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wanawake kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya afya ya uzazi sambamba na magonjwa yatokanayo na mfumo wa maisha.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa TAMWA, Bi. Alakok Mayombo alisema washiriki wa mafunzo hayo watajengewa uwezo kuhusu afya ya uzazi pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii.
“Katika kipindi cha siku mbili za mafunzo Tumezungumza na marafiki wa TAMWA Narayana hospital ambao wamekubali kutoa elimu ya afya uzazi kwa wakina mama kupitia kipengele chao cha awareness kuhusu hasa magonjwa ya kansa" Alisema Bi. Mayombo.
Alisema kupitia elimu ambayo itatolewa kwa washiriki hao itawawezesha kuwasaidia wao binafsi kama wakina mama pamoja na kuisaidia jamii kwa ujumla hasa katika jitihada za kupambana na kutatua matatizo yanayosababisha kansa kwa wakina mama.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEin-kGjBRikGFSJSCzxB-Q9iOOhd5SMejhd9WP6JE412SDIgELwyhbZP3l7ALtRjTYumuMYeDaI9IO-o7rTvAZZgA7joxbyJMNv1nr6u_iUDOdwH6ReNcrfCcXVC__QvoP3Yg0albSEjBLs/s640/IMG_20190405_101036%257E2.jpg)
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Tamwa, Bin Rose Reuben Akizungumza wakati wa ufunguzi huo alisema nje ya ya mafunzo kuhusu afya ya uzazi kwa wakinamama pia watatoa elimu kuhusu matumizi ya mtandao kwasababu unapotumia mitandao ya kijamii lazima utambue sheria ya maudhui ya mtandao pamoja na sheria za vyombo vya habari katika mitandao ya kijamii.
“Lengo letu ni kujiongezea ujuzi katika maeneo haya na hii watu ambao watakuja kutusaidia kutoa mafunzo hayo ya matumizi ya mtandao ni watu wa TCRA”. Alisema Bi. Reuben.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjmW4Z9HfQMeXNQkuO4PJHQraYgWqQXyn-R8frRrx6xWCq8fGdpwRuOkSdQTi20Q69bCWGjcEwsGDRJEgJWYCwihHN0WlCNPv35VWzBYDOZkdFN0KJbkE0ZOcSXy2KsLBC9Kmw9Tmk1MVXE/s640/IMG_20190405_104525%257E2.jpg)
Nae daktari kutoka Hospitali ya Narayana Bw Limbanga Freddie alisema tafiti zinaonyesha kumekuwepo na ongezeko kubwa la wagonjwa wa kansa kutokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha pamoja na kutofanya mazoezi, kutokufanya kazi ngumu na kutumia vyakula ambavyo ni hatari katika afya yake.
“Tafiti zinaonyesha kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani kutokana na kutokufatilia kanuni za afya ikiwemo ulaji usiofaa, kutokufanya mazoezi, ulaji wa vyakula vya kufungwa jambo ambalo linaelekea kuongezeko la saratani nchini. Alisema Dkt. Freddie.
Nae daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama kutoka nchini India Dkt. Rohit Ranade alisema tatizo la kansa ya kizazi ni moja ya changamoto kubwa kupitia mafunzo hayo ambayo watatoa elimu ambayo itasaidia kupunguza uwepo wa magonjwa ya kansa hiyo kwa wakinamama.
No comments