Vijana Dini Ya Kiislamu Mkoa Wa Dar Wamtaka Zitto Kuomba Radhi Kufatia Kupandisha Bendera Kwa Neno Tukufu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjD0rm4MkfCcYWlGYr_jed5DIlF7JFVpegnVzMm23ihql8iXmSLa4Hq6KfqwDd9JhZ6ChO7lx5kcQzrrwO36JvmxhagS6YaUkOliG39HdSUxNo4DmpexX4ECwykuNc6dkSG8-tPpQapx4U6/s640/IMG_20190327_102743.jpg)
Vijana wa dini ya kiislam mkoa wa dar es salaam kupitia Naibu Amir wa shura ya maimamu ambaye pia ni Amir wa vijana, Shekh Juma Ramadhani Juma wamelaani na kumtaka kiongozi wa chama cha ACT wazalendo Mhe Zitto Kabwe kuomba radhi waislam kufatia kauli yake aliyoitoa katika mkutano na waandishi wa habari 26 mwezi huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam alisema kiongozi huyo wakati akiongea wakati aijibu barua ya Msajili wa vyama vya siasa nchini ambayo imewataka kutoa maelezo kwann wasichukuliwe hatua kufatia kusambaa kwa video za wanachama wa chama hicho wakichoma bendera na kadi za chama cha wananchi CUF pamoja na kutamka neno Takbir wakati wakipandisha bendela ya chama icho visiwano zanzibar.
"Demokrasia au chama chochote cha siasa akifungamani na Dhehebu lolote la dini kutokana na vyama hivyo kuwa na katiba zao na sheria zao hivyo kitendo cha kutumia neno takatifu katika zoezi la kupandishaji wa bendela ya chama hicho ni kitendo cha kulaaniwa na kila mpenda amani na umoja uliopo nchini" Alisema Shekh Juma.
Alisema kitendo cha kiongozi huyo kuongea na waanshi wa habari na kusema kitendo hicho hakina madhala na kumtaka mufti na viongozi wa dini kushauri msajili wa vyama vya siasa nchini ni cha ajabu ukizingatia matamshi ayo ya natoka katika kimya cha Mhe zitto ambae pia ni muumini wa dini ya kiislam.
Aidha shekh Juma aliongeza kuwa kitendo cha kutumia neno hilo tukufu si chakufumbiwa macho kwani kinaleta picha kuwa tayali nchi inaweza kuwa dola ya kiislam japo wote ni mashahidi kuwa nchi yetu ina dini tofauti lakini tumekuwa tukiisha kwa amani umoja na mshikamano katika kipindi chote hivyo kinachofanywa na chama hicho ni kutaka kuvuluga amani na umoja uliopo nchini.

No comments