Breaking News

CUF Yawafungulia Kesi Waliofanya Uhalibifu Wa Mali Zake Zanzibar

Chama cha Wananchi (CUF) kimewataka wanachama visiwani Zanzibar kutojiusisha na vitendo vya uharibifu pamoja uvunjifu wa amani mbavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watu.

Kutokana na vitendo ambavyo vimefanya na baadhi ya watu Zanzibar, CUF imefungua kesi namba 16 ya mwaka 2019 katika mahakama ya Vuga dhidi ya watu wote waliohusika kushusha bendera na kubadilisha rangi za ofisi za Chama hicho kwa kuzipaka rangi ya chama cha ACT wazalendo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman khalifa alisema vitendo vinavyofanywa ni kinyume na sheria pamoja na kuvuruga amani.

"Ofisi zote ni mali ya CUF, na hiki Chama ni Taasisi na sio cha mtu mmoja, hivyo watu wote waliofanya uharibifu wa kuchoma moto bendera, kubadilisha rangi watachukuliwa hatua za kisheria" alisema Khalifa

Alifafanua kuwa mpaka sasa tayari wamekushany ushahidi wa matukio yote yaliofanyika pamoja na majina ya watuhumiwa ambao watafikishwa mahakamani.

Alisema kuwa hakuna ofisi yoyote ya CUF ambayo ilinunuliwa na mtu binafsi au mwanachama kwani taarifa zote za mali za CUF zipo kwa msajili wa vyama vya siasa.

"Mpaka sasa tayari kuna ofisi zaidi 100 zimefanyiwa hujuma na nitahakikisha na simamia mali zote za chama" alisema Khalifa

Hata hivyo alieleza kuwa ziara ya aliyekuwa  katibu Mkuu wa CUF Maalif Seif Sharif Hamad mjini Pemba ilikuwa ni kujitambulisha kwa wananchi, kuwa amejiunga na ACT Wazalendo pamoja na kuwashawishi kumfata.

"Ile ziara ya pemba sio ya kujenga Chama Cha ACT Wazalendo ilikuwa ni kujitambulisha kwa wananchi pamoja na kuwaomba wanachama kumuunga mkono" alisema Khalifa

Katika hatua nyingine amewataka wabunge wote wa CUF kuendeleza ushirikiano na Chama chao kwa kufika ofisi na kupeana mikono na kukijenga Chama.

"Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba alishawasamehe wabunge wote kwa sasa kinachotakiwa kuwa na ushirikiano wa pamoja kutokana wabunge wamechaguliwa na wananchi" alisema Khalifa. 

No comments