Breaking News

Mchungaji MASHIMO: Atoa Neno Kwa Diamond Planumz

Mchungaji wa Manabii na Mitume Komando Mashimo amemtaka msanii maarufu wa mziki wa kizazi kipya nchini Nasib Abdul (Diamond Planumz) kuachana na tofauti zilizopo kati yake na mzazi wake na kujitokeza kumsaidia hususani kipindi hiki ambacho mzazi wake huyo anaumwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam juu ya maono ya kiunabii ambayo ameonyeshwa na mwemyezi Mungu, Mchungaji Mashimo alisema kumekuwepo na kutokuelewana kati ya msanii huyo na mzazi wake wa kiume kwa kipindi kirefu ikiusishwa na kitendo cha mzazi wake huyo kumtelekeza akiwa mdogo.

"Kumekuwepo na taarifa kuwa msanii huyo alitelekezwa na mzazi wake huyo kipindi akiwa mdogo jambo ambalo limepelekea kutokuwepo na maelewano kati yao, ivyo nitoe rai kwa Nasib (Diamond) kujitokeza na kusamehe yote yaliopita na badala yake amsaidie hususani kipindi hichi ambacho mzee wake huyo anaitaji sana msaada kutokana na kuumwa"Alisema Mchungaji Mashimo.

Alisema kwa mujibu wa maono ambayo amepokea msanii huyo asipojitokeza na kuanza kumsaidia mzazi wake huyo yupo katika hatari ya kupatwa na mabalaa siku sio nyingi ivyo kumtaka kutokupuuza ushauri wake huu.

"Ata vitabu vitakatifu vya dini vyote vinasisitiza kuwaheshimu wazazi wote wawili ili upate baraka na kheri duniani, ivyo nazungumza haya sio kwamba sitambui changamoto alizokutana nazo kipindi ambacho mzazi wake alishindwa kutekeleza wajibu wake bali naongea kama kiongozi wa dini na maandiko yanasema na kusisitiza kuwaheshimu wazazi wote" Alisema Mchungaji Mashimo.

Aidha mchungaji mashimo aliongeza kuwa kitendo cha msanii huyo kuendelea kushirikiana na mama yake tu wakati mzazi wake wa kiume akiwa anaumwa na kuhitaji msaada kutoka kwake na uwezo wa kumsaidia anao katika maono ya kinabii imemwonuesha kuwa sio jambo jema na asipobadilika basi ajiandae kukutwa na mabalaa ikiwepo kufilisika mali zote alizonazo.

Pia mchungaji Mashimo amewaomba viongozi wa dini hususani dini ya kiislam kujitokeza kujaribu kusuluhisha mgogoro huo kwani wanayo nafasi kubwa ya kuweza kumshawishi msanii huo kubadili uamuzi wake na kuanza kumsaidia mzazi wake huyo. 

No comments