Makamu Wa Rais Mhe Samia kufungua kongamano La Saba La Maonyesho Ya Afya Jumuiya Ya Afrika Mashariki
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSstM7MMyieoYudxIksCtTCvo8WJqt_lRPx1sy1nYFe8NMclT_zALLJmNtjBxh_KcSlIpSkfpU9Ij1laqUs4go2jNYMX9MXDNSb5IzNKQ_9VMj1LkqsNJvSw7oh_ffPF94k0v1nL6RNhXI/s640/Kaimu+Katibu+Mkuu+wa+Wizara+ya+Afya%252C+Maendeleo+ya+Jamii%252C+Jinsia%252C+Wazee+na+Watoto%252C+Prof.+Mohammad+Kambi.jpg)
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa Kongamano na Maonesho ya Awamu ya Saba ya afya, sayansi na Biashara Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na maonyesho ya kimataifa ambayo yamepangwa kuanza Machi 27 hadi 29 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mapema leo jijini humo na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhamad Kambi wakati akitoa taarifa ya kongamano na maonesho hayo yatayofanyika kwa siku tatu.
Amesema kuwa kongamano hilo ni la saba na kwamba lengo ni kubadilishana mawazo kati ya washiriki ya namna ya kutumia Tekolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika uendeshaji wa huduma za afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC).
“Maandalizi yameshafanyika kikao cha mwisho kilifanyika Burundi baada ya miaka kitafanyika Kenya tunatarajia Samia atalifungua Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere” Alisema Profesa Kambi.
Amebainisha kuwa kongamano hilo litakwenda sambamba na maonesho ya Tehama huku akiwasisitiza wananchi kushiriki kupata fursa zitakazowasilishwa.
Amesisitiza kuwa matumizi ya Tehama kwa kiasi kikubwa yamesaidia katika utoaji tiba, ufuatiliaji wa magonjwa ya binadamu pamoja na uendeshaji wa hosptali kwenye ukusanyaji na udhibiti wa mapato.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRDeekJleZHVf9aMfoSa3KNjC_kd_u-qr3GbfKbShAcBBKtNnz1C3NKG6BuiZrJvfMrMqzFSYIJlnKaSHAF751A8B6uaKpagPUEWGsvr738XAiKjf3Kn0K6CD_KhmzIbb0CHklbNs05lGZ/s640/KIBIKI+EAC.jpg)
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Utafiti katika Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EARC), Profesa Gibson Kibiki amesema kuwa kongamano na maonesho hayo ni mpango mkakati wa miaka 10 na kwamba utaanza kutumika siku ya ufunguzi.
Profesa Kibiki amesema kuwa kongamano litaangalia namna bora ya kutumia Tehama kwenye sekta ya afya ili kufanikisha mpango mkakati huo.
Amefafanua kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni Teknolojia kwa ajili ya kubadili mifumo ya afya ili kutimiza malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN).
Naye Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Profesa Eligius Lyamuya amesema walipokea mada 200 na kuzichuja kubakia 90 ambapo 10 ni mtambuka huku 80 zikitarajiwa kuwasilishwa kwa makundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa nchini (NIMR), Profesa Yunus Mgaya amesema kongamano hilo litashirikisha nchi sita wanachama wa EAC na kwamba wananchi wataofika kushuhudia wataona namna Tehama inavyotumika kwenye sekta hiyo.
No comments