Wataalamu Wa Ununuzi Na Ugavi Waaswa Kufata Maadili.
Mkurugenzi Wa Maendeleo ya Taaluma Bodi Ya Ununuzi Na
Ugavi (PSPTB) Bw. Ally Songoro akikabidhi Cheti kwa mmoja wa wahitimu wa
mafunzo ya siku 5u ya tafiti Jijini
Dar es salaam.
Dar es salaam:
Wataalam Wa Manunuzi Na Ugavi nchini wametakiwa
kutekeleza majukumu yao kwa kufatua maadili ya taaluma hiyo sambamba na kufanya
utafiti kutokana na umuhimu wao katika kutelekea azma ya serikali ya uchumi wa
viwanda.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafuzo
ya siku tano yaliowakutanisha maofisa ugavi na wanunuzi kutoka nchi nzima Mkurugenzi
Wa Maendeleo ya Taaluma Bodi Ya Ununuzi Na Ugavi (PSPTB) Bw. Ally Songoro alisema
kama watatekeleza majukumu yao vizuri na kufata maadili itaisaidia kuondoa
mianya ya ubadhilifu.
Alisema swala la kuwa na maadili ni swala muhimu sana
kutokana na umuhimu wa wataalam hao kwani zaidi ya asilimia 80 ya matumizi ya
serikali yapo katika upande wa manunuzi.
“Maadili ni swala muhimu sana wao kama wataalam
watekeleze majukumu yao vizuri kwa kufanya utafiti sio wanasoma na kufanya
research harafu utendaji wao uwe tofauti” Alisema Bw. Songoro.
Aidha Bw. Songoro amewataka wataalam wote manunuzi na
ugavi nchini kuhakikisha wanasajiliwa na bodi hili kuweza kufanya kazi zao
vizuri, kutofanya hivyo ni kukiuka sheria na taratibu za bodi.
Jumla ya washiriki 113 kutoka Tanzania Bara Na Zanzibar
wameshiriki mafunzo hayo ya siku 5 ya utafiti na kupewa vyeti vya kuhitimu
mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku 5 ya utafiti yalitolewa
na Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa na wataalam wa bodi hiyo Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Wa Mafunzo Bw. Amani Ngonyani akifafanua
jambo katika mafunzo ya siku 5 ya utafiti
yalitolewa na Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) jijini dare s salaam.
Wahitimu wa mafunzo ya siku 5 ya utafiti yalitolewa
na Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kumalizika mafunzo hayo jijini Dar es salaam.
No comments