Taarifa Kutoka Nec Kwa Vyama Vitakavyoshiriki Uchaguzi Wa Marudi Kinondoni Terehe 17
Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Bw. Ramadhan Kailima
amevikumbusha vyama vya siasa vitakavyoshiriki Uchaguzi Mdogo wa Februari 17
kuwasilisha majina ya mawakala wao kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi
Wasaidizi wa Uchaguzi kabla ya siku ya mwisho ambayo ni kesho (Tarehe 10).
Amesema hii ni
kwa mujibu wa Kifungu Na. 57(2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Sura ya 343)
na Kifungu Na.58 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa (Sura ya 292).
Uchaguzi Mdogo wa Februari 17 utahusisha Majimbo Mawili (2) na Kata Tisa (9).
No comments