TRL Yatangaza Ratiba Ya Treni Kwenda Bara Sasa Kuanzia Dodoma.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Uendeshaji wa TRL Focus Sahani akizungumza na waandishi wa habari(hawapo
pichani) makao makuu ya kampuni ya Reli (TRL) jijini Dar es Salaam.
*****
KAMPUNI ya relini nchini( TRL) imesema sasa safari za
treni zitaanzia Dodoma kwenda Kigoma , Mpanda na Mwanza.
Hatua hiyo imekuja kufuatia huduma za usafiri wa reli kutoka
Dar es Salaam kwenda bara kusitishwa kutokana na mafuriko ya mvua zinazoendelea
kunyesha sehemu mbalimbali kuharibu
miundombinu ya reli kati ya stesheni za Kilosa na Gulwe.
Hayo yemeelezwa na kaimu naibu Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji wa TRL, Bw.Focus
Sahani akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya shirika hilo jijini dar
es salaam kuhusu ratiba mpya ya huduma za treni kuanzia leo tarehe 16 Januari.
“Uongozi baada ya kufanya
tathmini hali ya miundombinu ya maeneo mengine yaliosalama imeamua kuhamishia
huduma ya usafiri wa treni kutokea Dodoma kuanzia Januari 16, 2018,” Alisema Bw.
Sahani.
Akitaja ratiba hiyo, Sahani alisema
treni ya abiria kutoka Dodoma itaondoka saa moja usiku siku ya Jumanne na
Ijumaa kwenda Kigoma, Mwanza na Mpanda ambako inatarajiwa kuwasili Mwanza saa
12 jioni siku ya Jumatano na Mpanda saa 12 jioni na Kigoma saa 12:30 jioni.
Treni kutoka Mpanda, Mwanza na
Kigoma zitatoka huko siku za Jumapili na Alhamisi tu. Mpanda itatoka saa 1:00
asubuhi, Mwanza itatoka saa 2:00 asubuhi na Kigoma itatoka saa 1:30 asubuhi.
Treni hizo zinafika Dodoma siku ya saa 12:30 jioni.
Wakati huo huo alisema treni
pekee ya kutoka Tabora kwenda Mpanda kurejea Tabora siku za Jumatatu, Jumatano
na Jumamosi. Itakuwa inaondoka Tabora saa 12 asubuhi na kuwasili Mpanda saa
12:32 jioni. Itaondoka Mpanda kurejea Tabora saa 1:00 asubuhi na kuwasili saa
12:38 jioni.
Alisema mafundi wa kampuni hiyo
wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa kazi ya ukarabari na kurejesha
katika hali yake maeneno yote inaendelea kwa kasi kati ya Kilosa na Gulwe hili
kuweza kurejesha safari kama hilivyokuwa awali.
No comments