Majina Ya Wafungwa 12 Waliopewa Msamaha Na Rais Dkt Shein
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjAe9DA_y9NSrDa8dGKBguUehyphenhyphen6zWosmVXLZOkgPLglQcTvOhnDdldzm8qJBCYeyAZLR_WUjJhHSuI5oVdim0_-Nx5y5VTR79g5e4QWuQ50sS7Jh1XsPELo16CD-cmnnBXY86iGGtcJSDWD/s640/1.jpg)
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na
Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein, ametoa msamaha kwa wafungwa 12 ikiwa
ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Dkt Shein ametoa msahama kwa
wafungwa hao ambao walikuwa wamehukumiwa kwa makosa mbalimbali.
Msamaha huo umetolewa kwa mujibu wa
ibara ya 59 ya Katiba ya Zanzibari ya mwaka 1984 ambayo imempa Rais mamlaka ya
kutoa msamaha kwa wafungwa.
Msamaha huo unatolewa kwa wafungwa
kama nafasi ya wao kuanza kuishi maisha mapya na kuachana na vitendo vya
kihalifu.
Wafungwa waliopewa msamaha huo ni;
1.
Abdul-Aziz Abdalla
2.
Omar Abdalla Nuhu
3.
Ali Khamis Mrau
4.
Mussa Ali Vuai
5.
Hassan Seif Khamis
6.
Nassor Abeid Issa
7.
Jihadi Jalala Jihadi
8.
Edward Jemeria Magaja
9.
Sleiman Abdalla Amir
10.
Mtumwa Khamis
11.
Said Seif Omar
12.
Masoud Seif Nassor
Katika hatua nyingine, raia wengi 74
wa Zanzibar (baadhi yao wamefariki) wametunukiwa medali na Rais Dkt Shein
kutokana na mchango wao mkubwa katika mapinduzi na pia kuleta maendeleo katika
visiwa hivyo.
Miongoni mwao, raia 43 wamepewe
medali za mapinduzi huku wengine 31 wakipewa medali za mfano kwa utumishi wao
uliotukuta kwa wananchi.
No comments