POGBA ataka kulipwa zaidi ya Sanchez Man Utd
Paul
Pogba
MCHEZAJI
wa Manchester United, Paul Pogba sasa anataka kulipwa mshahara mara mbili ya
anaoupokea sasa wa paundi laki mbili kwa wiki na klabu yake hiyo.
Hatua
yake hiyo ni kutaka mshahara wake ufanane au uzidi wa mchezaji mpya wa
timu hiyo Alexis Sanchez atakayekuwa akilipwa paund laki nne na nusu kwa wiki.
Wakala
wa mchezaji huyo, Mino Raiola amesema kwa sasa thamani ya malipo ya mshahara wa
mchezaji mwenye ubora kama wa Pogba ambaye ni raia wa Ufaransa umeongezeka
maradufu katika dirisha la usajili na kwamba Pogba anastahili kulipwa zaidi ya
paundi laki nne kwa wiki.
Kiungo
huyo mbunifu aliyenunuliwa mwaka jana kwa paundi milioni 89 kutoka klabu ya
Juventus ya Italia amebakisha miaka mitatu ya mkataba wake wa kuichezea timu ya
Man Utd.
Wakala
Raiola amesema mkufunzi wa Manchester united, Jose Mourinho anajua umuhimu wa
mchezaji huyo na ili ambakishe klabuni hapo hana budi kumuongezea mkataba wa
muda mrefu na kumlipa mshahara mnono wa kumfanya Pogba awe ni mwenye furaha.
Source Mashirika ya Mtandao
No comments