Picha Za Tundu Lissu Alivyowasili Na Kupokelewa Ubelgiji
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyrTkIPvbTWnd21gi4v8ndDszUo1gTtynwvoGcLQqRwZFkpHZfPBWP7t0PQJDCRua14Y3gzLPkVYhceIHTlXgPCQ1miSnT-GXwXJpml_GWfmRYwjdnVWUToTSOW_IEoUyvVBHXCWxi5O5l/s640/1.jpg)
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Antipas Lissu amewasili katika uwanja wa ndege jijini Brussels, nchini Ubelgiji
ambapo amepelekwa kwa ajili ya awamu ya tatu ya matibabu yake yatakayohusisha
mazoezi ya viungo.
Tundu Lissu amewasili jijini hapo akitokea katika Hospitali ya
Nairobi, nchini Kenya alikokuwa anapatiwa matibabu kwa muda wa takribani miezi
minne sasa, kutokana na kushambuliwa kwa risasi.
Mbunge Tundu Lissu, ambaye pia ni
Mnadhimu Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni, alishambuliwa kwa risasi na watu
wasiojulikana, alipokuwa akitokea Bungeni, majira ya saa 7 mchana, karibu na
nyumbani kwake Area D, Mjini Dodoma.
Kwa Mujibu wa taarifa ya madaktari
waliokuwa wanamtibu, walieleza kuwa jumla ya risasi 16 zilimpata Tundu Lissu
mwilini mwake, na wamefanikiwa kuzitoa, isipokuwa moja ambayo iko nyuma ya uti
wa mgongo wake.
Tundu Lissu alieleza kuwa wataalamu
na madaktari wake walishauri kuwa risasi hiyo ni hatari zaidi kama ikitolewa
kuliko ikibaki ndani ya mwili wake, kutokana na eneo ilipokwama.
==>Picha
za Mbunge Tundu lissu alipowasili jijini Brussels kwa ajili ya matibabu zaidi.
No comments