List Ya Kampuni Zilizo Na Idadi kuibwa Waidawa Sugu Wa Bodi Ya Mikopo
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkFsWIzZnfOk9UEjmrlTaobT1clHCsWMEilHTfbESLqMRO6uW84kBKXU0V4R-hLp4Mfx10sJ9w9Q-enMuLZbYG15GOeyILSdpttnRm6ocrBpSIAnTSBDYbsT_BmD-uQdbKd5t0_Goq7Pk/s640/MIKOPO-HESLB.png)
Bodi Ya Mikopo Ya Elimu Ya Juu (HESLB)
Imeanika Majina 57 Ya Kampuni, Shule, Vyuo Na Mashirika Ambayo Waajiri Wake
Hawawasilishi Makato Ya Wanufaika Wa Mikopo Kwa Wakati.
Uanikaji Wa Majina Hayo Kupitia Tovuti
Ya HESLB Umekuja Siku Mbili Baada Ya Kutangaza Kufanya Hivyo Jumatano Iliyopita.
Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo,
Phidelis Joseph Alisema Kabla Ya Kuanza Kuwasaka Wanufaika 119,497 Ambao
Hawajarejesha Mikopo Yao, Wataanika Majina Yao Hadharani.
Miongoni Mwa Kampuni Zilizotajwa Ni
Pamoja Na Taasisi Ya Tiba Ya Mifupa (MOI), Mamlaka Ya Majisafi Na Majitaka Dar Es
Salaam (Dawasco), Baraza La Sanaa La Taifa (Basata), Mamlaka Ya Chakula Na Dawa
(TFDA), Shirika La NSSF, Mamlaka Ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA), Puma
Energy Limited, Mamlaka Ya Udhibiti Wa Usafiri Wa Nchi Kavu Na Majini (Sumatra),
Bohari Kuu Ya Dawa (MSD) Na Shirika La Taifa La Maendeleo (NDC).
Zipo Pia Shule Za Sekondari Ambazo
Waajiri Wake Hawapeleki Fedha Kwa Wakati Licha Ya Kuwakata Wafanyakazi Wao.
Akifafanua Kuhusu Muda Wa Kuwasilisha
Fedha Za Makato Ya Wanufaika, Mkurugenzi Mtendaji Wa HESLB, Abdul-Razaq Badru Alisema
Kila Mwajiri Ana Wajibu Wa Kisheria Wa Kuwasilisha Makato Ya Wanufaika Wa
Mikopo Ya Elimu Ya Juu Kwa Bodi Ndani Ya Siku 15 Baada Ya Mwisho Wa Mwezi.
“Baadhi Ya Waajiri Wamekuwa Hawafanyi
Hivyo Na Kuilazimisha Bodi Ya Mikopo Kuanza Kuwasaka Kwa Nguvu.
“Katika Msako Huu Hatutamuacha Mtu Au
Mwajiri Yeyote Anayekiuka Sheria Iliyoanzisha Bodi,” Alisema Badru.
Kaimu Mkurugenzi Wa Habariwa HESLB, Omega
Ngole Alisema Kwamba Idadi Ya Wanaokwenda Kulipa Madeni Yao Imeongezeka.
Alisema Kwa Kawaida Ofisi Zao Za Kanda
Zilizopo Arusha, Dodoma, Mwanza Na Zanzibar Hupokea Wadaiwa Wapya Kati Ya 15
Hadi 25 Kwa Siku, Lakini Kuanzia Jana Wamepokea Zaidi Ya 50.
Akizungumzia Zaidi Kuhusu Ofisi Za
Makao Makuu, Ngole Alisema: “Tunapokea Wadaiwa Wapya Wanaotaka Kulipa Zaidi Ya
300 Ambayo Haikuwa Kawaida, Wapo Na Viongozi Ambao Majina Yao Yapo Kwenye
Orodha Ya Wadaiwa, Wamemaliza Leo.”
Alisema Kwamba Wanawashukuru Wote Kwa
Kutimiza Wajibu Wao Kwa Kuwa Fedha Hizo Zitatumika Kwa Ajili Ya Kuwasomesha
Wahitaji Wengine.
No comments