MTULIA Aomba Radhi Kwa Kuigaragaza Vibaya CCM 2015 Akiwa UKAWA
![](https://3.bp.blogspot.com/-Hp9iSDRBF-w/WmTd3Y57rPI/AAAAAAAAW20/M8qM62Cc1mI6xv_IXRrxvFvvC2aquFAgQCLcBGAs/s640/mtuliaa.jpg)
Mgombea
ubunge jimbo la Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia amewaomba radhi wanachama wa
chama hicho tawala kwa ushindi wa kishindo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2015 akiwa CUF.
Mtulia
ametoa kauli hiyo leo Januari 21, mwaka 2018 wakati akitambulishwa kwa
wanachama wa chama hicho wilaya ya Kinondoni.
Mwaka
2015, Mtulia alishinda ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF, lakini Desemba 2
mwaka jana alijivua uanachama wa chama hicho na kuhamia CCM, hivyo kupoteza
sifa ya ubunge.
Hata
hivyo CCM kilimpitisha kugombea ubunge katika jimbo hilo.
Source Mwanachi
No comments