LOWASSA Akutana na FREEMAN MBOWE Kumpa Mrejesho Ziara Yake Ikulu
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3dxo58XYlUT3VpTEZhcSS5N2IpqzQGti5XmH7fFMV7ql3NWnV9N6to5REyTqwg4fl6c7gX8QAqceY07GcA_prq33e7bqtUdAtwOYFQCS7ZDpOIsX07sHl7QAKIY3kG-xy2ljlFAFyz-gc/s640/1.jpg)
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa
amekutana na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kumpa mrejesho wa
alichozungumza na Rais John Magufuli.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na
Msemaji wa Lowassa imeeleza kuwa kumekuwa na waraka na taarifa nyingi za
kupotosha umma kuhusu ziara ya Lowassa kwenda Ikulu na nyingine zikisemwa
zimetoka kwa msemaji wake.
“Taarifa zote hizo siyo kweli na wala
siyo rasmi kutoka ofisini kwa Mh Lowassa. Baada ya ziara ile, Mhe Lowassa
alikutana na mwenyekiti wa chama chake, Mhe Freeman Mbowe na kumpa mrejesho wa
yaliyojiri Ikulu.”
“Kumekuwa na taarifa nyingi kwenye
mitandao zikiwemo kufunguliwa kwa akaunti mbalimbali feki , taarifa zote hizo
zipuuzwe kwani zina lengo la kupotosha kwa malengo wanayoyajua wapotoshaji hao
pamoja na mawakala wao,”
“Taarifa rasmi zitatolewa kwa njia
rasmi na watu wenye mamlaka hiyo.poleni kwa usumbufu wote.”
***********
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDxzsrtf8B2C91ibpM1UunywwoA4hHtGB6_SoliLVRpe9xZ9ePfh-UG5ZNq5_6NuA903BDkC2umCV25aT0efxR9uhqY_9TncXog1w4CpciWqAhcNCVbUlPLLfuBXnMgR2pLlYUg_sdImhS/s640/1.jpg)
No comments