Jipu La AIRTEL,TTCL Laiva.. Ripoti Ya Kamati Ya Uchunguzi Yatua Kwa JPM... Serikali Imeingizwa MKENGE
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip
Mpango amewasilisha kwa Rais John Magufuli taarifa ya kamati aliyoiunda
kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel na kueleza jinsi Serikali
ilivyoingizwa mkenge.
Taarifa hiyo imewasilishwa
baada ya Rais Magufuli kutoa agizo la kufanyika hivyo Desemba 20 mwaka jana.
Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Dk
Mpango alisema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu
Tanzania (TTCL) kwenda Celtel, baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel
ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu.
Kufuatia ukiukwaji huo Dk Mpango
amesema Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua
kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili
nchi iweze kupata haki yake.
“Lakini niwaambie Watanzania yale
ambayo tumeyaona ni machafu sana, ni mambo ya hovyo kabisa, nchi yetu kwa
kifupi tuliingizwa mkenge, ni fedha nyingi zimepotea kwa hiyo sisi katika
majadiliano haya lengo letu litakuwa ni kuhakikisha Watanzania wanapata haki
yao,” alisema Dk Mpango.
No comments