TGNP Yawanoa Wanawake Namna Ya Kuingiza Masuala Ya Jinsia Katika Biashara Wanaofanya Kazi Mipakani
Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) na Taasisi ya mafunzo ya jinsia (GTI)
wameanza mafunzo ya siku tatu kwa ajili ya kuangalia namna ya
kuingiza masuala ya jinsia katika biashara kwa wanawake wafanyabiashara wa
mipakani na wadau wake.
Akizungumza jijini DAR ES SALAAM,
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP BI.LILIAN LIUNDI amesema kuwa mafunzo hayo
yamewakutanisha washiriki 35 wakiwemo maofisa wa serikali kutoka mipaka
tofauti, Asasi za kiraia pamoja na wafanyabiashara wanawake wanao jishughulisha
na biashara mipakani.
Aidha amesema mafunzo hayo ni
mwendelezo na yana lengo la kuwajengea uwezo washiriki ili waweze kukabiliana
na changamoto katika biashara sambamba na kuimarisha uwezo katika uingizaji wa
masuala ya jinsia katika sera,mipango,bajeti miundo na michakato yote inayohusu
biashara za mipakani.
Amebainisha kuwa utafiti uliofanywa
na kituo cha sera za biashara Afrika (ATPC) umeonyesha biashara inatoa ajira
kwa asilimia 60 ya wanawake katika biashara zinazofanyika katika nchi
zilizopo chini ya jangwa la sahara ambapo asilimia 70 na 80 ya
wanawake hao wamejikita katika biashara isiyo rasmi. `
Kwa upande wake mshauri wa masuala ya
jinsia na maendeleo BW.SULTAN MHINA amesema kuwa zipo changamoto
nyingi zinazoikabili nchi ya DEMOKRASIA YA CONGO hasa katika mahusiano ya
kijinsia kutokana na ukosefu wa uzingatiwaji wa sheria.
No comments