Breaking News

Washindi Wa Amua Accelerator Wapatikana, kila moja apata Zawadi Ya Dola 6,000

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akizungumza katika hafla ya kuwatangaza washindi wa mradi wa AMUA Accelerator.
Washindi wa shindano la Amua accelerator wakiwa katika picha ya pamoja na majaji na waandaji wa mradi wa AMUA Accelerator.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu nchini (UNFPA) Dkt. Hashina Begum akizungumza katika hafla ya kutangaza washindi wa mradi wa AMUA Accelerator.
Mmoja wa majaji wa mradi wa AMUA Accelerator akitoa maelezo kuhusu mradi wa AMUA Accelerator.
 Mwakilishi wa kikundi cha Harakati za lucy Bw, Gwamaka Mwabuka akitoa maelezo namna kikundi hicho kilivyobuni wazo lao na namna kitakavyotoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.
Mwakilishi wa kikundi cha e-Shangazi Debora Peter akitoa maelezo namna kikundi hicho kilivyobuni wazo lao na namna kitakavyotoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.
Mwakilishi wa kikundi cha Mkwawa Arts Space wakitoa maelezo namna kikundi hicho kilivyobuni wazo lao na namna kitakavyotoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.
Mwakilishi wa kikundi cha Maisha Package wakitoa maelezo namna kikundi hicho kilivyobuni wazo lao na namna kitakavyotoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.
Meneja Programu ya afya ya uzazi, mama na mtoto kutoka (UNFPA) Bi, Felista Bwana akibadilishana mawazo na majaji wa mradi wa AMUA Accelerator.
 Mwakilishi wa kikundi cha Harakati za lucy Bw, Gwamaka Mwabuka akipokea mfano wa hundi dola 6000 (Tsh Mil !3),kama moja ya washindi wa mradi wa  AMUA Accelerator.
Mwakilishi wa kikundi cha e-Shangazi Debora Peter akipokea mfano wa hundi dola 6000 (Tsh Mil !3) kama moja ya washindi wa mradi wa  AMUA Accelerator.
Mwakilishi wa kikundi cha Maisha Package akipokea mfano wa hundi dola 6000 kama moja ya washindi wa mradi wa  AMUA Accelerator.
Mwakilishi wa kikundi cha mkwawa Arts Space akipokea mfano wa hundi dola 6000 kama moja ya washindi wa mradi wa  AMUA Accelerator.
Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba akisikiliza maelezo kutoka kwa ya washirki wa mradi wa  AMUA Accelerator.



Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakifatilia mada mbalimbali zinazotolewa.

Wafanyakazi wa (UNFPA) wakibadilishana mawazo katika hafla ya hiyo ya kuwapata washindi wa mradi wa  AMUA Accelerator.
Afisa habari wa shirika la umoja wa mataifa Bi, Hoyce Temu akisikiliza maelezo kutoka kwa moja ya washirki wa mradi wa  AMUA Accelerator.

Dar es salaam
Washindi wanne wa mradi wa AMUA Accelerator ambao umelenga kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kukabiliana na mimba za utotoni wamepatikana ambapo kila kundi limepata zawadi ya dola 6,000 sawa na (Tsh. 13 milioni) ambazo watazitumia kuendeleza mawazo yao.
Akizungumza katika hafla ya kuwatangaza washindi wa AMUA Accelerator, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez alisema moja ya shughuli zinazoratibiwa na UN nchini ni kuwasaidia vijana kufikia malengo yao sambamba na kuwapatia elimu ya afya ya uzazi.
Alisema kupitia mradi huo ambao una malengo sawa na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) wao kama UN wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya kwa kutoa elimu ya afya ya uzazi vijana.
“Mradi huu ni sehemu ya mpango wetu wa kuhakikisha vijana wanafikia malengo yao, nawashukuru UNFPA kwa kuendesha mradi huu kwa ajili ya vijana Tanzania,” alisema Rodriguez
Aidha Bw. Rodriguez aliongeza kuwa Katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea uchumi wa kati kunahitajika kuwa na sera na mipango ambayo itaiwezesha nchi kuwa na uwiano wa umri na kutasaidia kuwepo kwa nguvu kazi na hasa vijana ambayo itafanya kazi na kusaidia uchumi kukua,
Alisema Mpango wa Innovation Accelerator unauhusiano na SDGs kama goli namba nne la kusaidia elimu, goli namba nane kwa kusaidia wajasiliamali na wabinifu,kupitia mradi huo UN Tanzania tutaendelea kushirikiana na Serikali kusaidia kumaliza changamoto za afya ya uzazi.
Mapema akizunguza katika hafla hiyo Meneja wa Mradi wa AMUA Accelerator,Bw. Adam Mbiyallu alisema mradi huo umeanzishwa ili kusaidia kutatua changamoto za afya katika jamii na zawadi ambazo watapewa washindi zitawasaidia kuendeleza mawazo waliyonayo kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya afya nchini.
Alisema washindi wanajaribu kutatua changamoto za maswala ya afya za uzazi hususani mimba za utotoni, tulitaka vijana waje na mawazo ya kijasiliamali na kibunifu ambayo yamejikitakatika kutatua changamoto za afya ya uzazi na jinsia.
Pia Bw. Mbiyallu aliongeza kuwa kupitia wazo hilo ambalo litatumika kama fursa ya ajira, na kuwataka vijana wanapoona fursa za aina hii wajitokeze kushiriki.
Jumla ya vikundi nne vimeibuka washindi kulingana na mawazo yao ya kibunifu ya kutatua changamoto ya afya ya uzazi na hususani kukabiliana na mimba za utotoni ni Harakati za Lucy, eShangazi, Maisha Package na Mkwawa Community Art Space.

No comments