Shule Ya St Judith Yaibuka Mshindi Wa Kwanza Katika Shindano La Wanasayansi Chipukizi 2017.
Mwenyekiti wa Bodi Ya (YST) Profesa Yunus Mgaya Akiongea katika Hafla ya
kukabidhi tuzo katika shindano la Wanasayansi Vijana (YST) jijini Dar es
Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa
Simoni Msangila Akiongea katika Halfa ya kuwatangaza washindi wa shindano la
wanasayansi Vijana (YST) jijini Dar es salaam.
Wadau kutoka makampuni mbalimbali wakifatilia utoiaji wa tuzo kwa
wanafunzi waliofanya vizuri katika utafiti wa kisayansi (YST) mwaka 2017
|
Moja ya washindi
wakikabidhiwa medani na kikombe katika mashindano ya wanasansi chipukizi (YST)
ambayo yamekutanisha wanafunzi kutoka shule za sekondari nchi nzima bara na
Zanzibar.
|
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini walioshiriki maonyesho ya ubunifu wa kazi za kisayansi kwa mwaka 2017 wakiimba wimbo wa taifa |
Wadau kutoka makampuni mbalimbali wakifatilia utoiaji wa tuzo kwa
wanafunzi waliofanya vizuri katika utafiti wa kisayansi (YST) mwaka 2017.
Dar es salaam
Wanafunzi wa Shule ya
Secondary ya St. Judith, Prosper Gasper na Erick Simon wametangazwa washindi wa
kwanza katika mashindano ya ubunifu wa kazi za kisayansi 2017 yaliyowakutanisha
wanafunzi kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar.
Wanafunzi hao ambao
walibuni teknolojia ya kuzuia ajali ya moto kwa kutumia simu walijishindia Tsh 1.8 Milioni wanatajiwa
kuwasilisha nchi nchini afrika kusini kushiriki mashindano ya wanasayansi
chipukizi duniani ambapo yatafanyika mwaka huu.
Akizungumza mara
baada ya kutangazwa kwa washindi wa shindano hilo mwanzilishi wa shindano la wanasayansi
vijana nchini (YST), Dk Gozibeti Kamugisha alisema mashindano hayo yamejikita
zaidi kuongeza na kutoa hamasa kwa wanafunzi hasa wa shule za secondary kupenda
masomo ya sayansi.
Alisema kupitia
shindano hilo ambalo linafanyika nchini kwa mara ya sita sasa limekuwa
likiwakutanisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini na kuwaleta pamoja ili
waweze kuonyesha kazi zao za kibunifu ambazo walizoziandaa.
Dk. Kamugisha aliongeza
kuwa kupitia kazi zao hizo za kibufu vijana hao wamekuwa wakipata wafadhili
ambao wamekuwa wakiwasaidia kuendeleza mawazo yao hayo jambo ambalo limekuwa ni
chachu kwa taifa kuweza kuwa na vijana walioiva katika maswala ya ki sayansi.
Alisema kupitia
shindano hilo vijana wengi wameanza kuwa na mwako wa kupenda na kutamani
kusomea masomo ya sayansi nchini ivyo kusaidia kuwezesha na `sera ya serikali
ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda.
Mashindano hayo
yamekutanisha zaidi ya wanafunzi mia kutoka shule za Secondary nchi nzima kushiriki
kuonyesha kazi zao za kiugunduzi wa kisayansi ambapo mshindi wa kwanza ataungana
na washindi wengine duniani katika fainali mashindano ya wanasayansi chipukizi
yanayotaraji kufanyika nchini afrika ya kusini.
No comments