TRA Msimfanye Nikatumbuliwa Na Rais Waziri Mwijage
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kutomfukuzisha kazi kwa uzembe wao uliopelekea nchi kupigwa na kupata hasara
kutokana na watu kuingiza cement kutoka nje ya nchi wakidai ni krinka.
Waziri Mwijaga alisema hayo jana
kupitia kipindi cha HOTMIX na ambapo alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kukagua krinka yoyote kutoka nje ya nchi.
"Mtu anatengeneza Krinka anauza
Kenya, sasa kama mtu anatengeneza Krinka Tanga anauza Kenya wewe unafuata nini
Pakistan? Hakuna krinka inatoka nje ya nchi ile ni Cement iliyokamilika TRA
wanashindwa kufanya kazi yao, narudia kusema hakuna krinka inaingia nchini
kutoka nje ile ni Cement kamili na anayepinga aje aniambie mimi, na kuanzia leo
TBS wasikague krinka yoyote kutoka nje ya nchi waingize ndani ya nchi bila TBS
kukagua, TBS ipo chini yangu sasa kama mimi naambiwa sitoshi na wa TBS
ajiangalie" alisema Mwijage
Aidha Waziri Mwijage alidai kuwa watu
wa Cement walikubaliana na DR Meru kununua hizo Krinka hapa hapa nchini
"Watu wa Cement walikubaliana
hapa na Dr. Meru, Twiga Cement ananunua Krinka, Simba Cement ....mwingine nani
ananunua krinka nyingine kutoka wapi, watu wanaleta cement iliyokamilika
wanasema Krinka sasa kuanzia leo TBS hawezi kukagua krinka yoyote kutoka nje ya
nchi, mpaka mamlaka iliyopo juu yangu sasa kama TRA walizembea tukapigwa juu
yao kwanini wanataka kuniharibiana kazi, eti bwana wanataka kuniharibia kazi
mimi" alisisitiza Waziri Mwijage
No comments