Mhe Samia Kuzindua kongamano la wanawake tarehe 26 mwezi huu Jijini Dar
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania he Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi wa jukwaa la uhamasishaji na uwezeshaji kiuchumi mkoa wa dar
es salaam utakaofanyika tarehe 26 mwezi huu.
Akizungumza na
waandishi mapema leo jijini dar es salaam Mkuu wa wilaya ya ilala Mhe Sophia Mjema
alisema uzinduzi huo ambao utawakutanisha wanawake zaidi ya 3000 kutoka katika
manispaa zote tano za jiji umelenga kuwakutanisha kushauliana namna ya kutatua
changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi.
Alisema jukwaa hilo
litatoa fursa kwa wanawake kutoka katika Nyanja mbalimbali za uzalishaji kukaa
pamoja na kubadilishana mawazo pamoja na kupewa mafunzo juu ya njia bora za
kuboresha biashara zao hili kujikwamua kiuchumi.
“kupitia jukwaa hili
wanawake kutoka manispaa zote za jiji la dar es salaam watakutana na kukaa pamoja
kubadilishana uzoefu na kupatiwa mafunzo namna wanavyoweza kutatua changamoto
wanazokutana nazo pamoja na kupatiwa ushauri wa kitaalam namna ya kuendesha shughuli
zao” Alisema Mhe Mjema.
Kwa upande wake
katibu mtendaji wa baraza la uwezeshaji (NEEC) Bi Beng’I Issa amewataka vijana
na wanawake kujitokeza kwa wingi siku hiyo hili kuweza kupatiwa elimu juu ya
kurasimisha biashara zao.
Alisema taasisi
mbalimbali zitashiriki Shirika la viwanda vidogo vidogo (SIDO), Shirika la
viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA), watatoa mafunzo na
kutoa vibali kwa wakina mama wanaendesha shughuli za uzalishaji pamoja na kuwapatia
vyeti baada ya kupatiwa mafunzo ya kuboresha bidhaa zao.
No comments