Breaking News

PROF. LIPUMBA AANZA KUPANGA SAFU YAKE CUF, AFANYA UTEUZI

Dar es salaam - Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba ameteua bwana Rajab Mbarouk Mohamed kuwa Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibiti ya chama hicho.

Pia amemteua, Juma Wandwi kuwa Naibu Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibit na wateule hao wataanza kazi mara moja na watathibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kikao kijacho na huku taarifa hiyo ikiongeza kuwa uteuzi wa wakurugenzi wengine utatangazwa kwa kadri uteuzi utavyokamilika.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo iliyotolewa Jan 13, 2025 na Kitengo cha Habari imefafanua kwamba, Prof. Lipumba amefanya uteuzi huo kwa kuzingatia Katiba ya CUF - Chama Cha Wananchi ya mwaka 1992 Toleo la 2019, Ibara za 91(1) na 92(1). 

No comments