Huu hapa Msimamo wa CLOUDS MEDIA baada ya Makonda Kugoma Kuomba Radhi
Leo ulifanyika mkutano na
Waandishi wa habari ukimuhusisha Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Ruge
Mutahaba, RC wa Dar es Salaam Paul Makonda na Jukwaa la Wahariri kuhusu
swala la kufungiwa kwa habari za Mkuu wa mkoa Paul Makonda.
Baada ya mkutano huo na mengine
yaliyojadiliwa na kauli zilizotolewa ikiwemo ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda
kusema hawezi kuomba radhi, Ruge Mutahaba amehojiwa na vyombo vya habari baada
tu ya mkutano huo kuisha na kueleza msimamo wa CLOUDS.
“Baada ya jambo la leo msimamo wa CLOUDS
MEDIA GROUP ni uleule tuliokua nao toka siku ya jumamosi baada ya kupatanishwa
na Mh. Rais, siku ile alivyotupatanisha sisi kama Watanzania hatukua na budi
zaidi ya kukubali na kurudi kwenye uhusiano wa kiuweledi.
“Leo tuliitwa kwenye kikao kwa kutegemea
labda kungekua kuna kingine cha ziada lakini” Amesema Ruge
No comments